پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Naml
سورهٔ ۲۷

An-Naml

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیه‌های ۳۸–۴۰

قَالَ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلْمَلَؤُا۟ أَيُّكُمْ يَأْتِينِى بِعَرْشِهَا قَبْلَ أَن يَأْتُونِى مُسْلِمِينَ ۳۸ قَالَ عِفْرِيتٌ مِّنَ ٱلْجِنِّ أَنَا۠ ءَاتِيكَ بِهِۦ قَبْلَ أَن تَقُومَ مِن مَّقَامِكَ ۖ وَإِنِّى عَلَيْهِ لَقَوِىٌّ أَمِينٌ ۳۹ قَالَ ٱلَّذِى عِندَهُۥ عِلْمٌ مِّنَ ٱلْكِتَـٰبِ أَنَا۠ ءَاتِيكَ بِهِۦ قَبْلَ أَن يَرْتَدَّ إِلَيْكَ طَرْفُكَ ۚ فَلَمَّا رَءَاهُ مُسْتَقِرًّا عِندَهُۥ قَالَ هَـٰذَا مِن فَضْلِ رَبِّى لِيَبْلُوَنِىٓ ءَأَشْكُرُ أَمْ أَكْفُرُ ۖ وَمَن شَكَرَ فَإِنَّمَا يَشْكُرُ لِنَفْسِهِۦ ۖ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ رَبِّى غَنِىٌّ كَرِيمٌ ۴۰

{38-40} Naye Suleiman alijua kwamba lazima watamjia. Kwa hivyo, akawaambia wale waliokuwa pamoja naye miongoni mwa majini na wanadamu, "Ni nani kati yenu atakayeniletea kiti chake cha enzi kabla hawajanijia nao wamekwisha salimu amri?" Ili tuvitumie vitu vyao kabla ya wao kujisalimisha kwa hivyo zikawa mali zao ni haramu kwetu. "Akasema Afriti mmoja katika majini," ambaye ni pepo mwenye nguvu sana na mkakamavu sana, "Mimi nitakuletea kabla hujainuka pahala pako hapo. Na mimi kwa hakika katika hilo nina nguvu na muaminifu." Na maana ya dhahiri ni kwamba Suleiman wakati huo alikuwa huko Sham, kwa hivyo inakuwa kati yake na Sabai ni umbali unaokaribia mwendo wa miezi minne. Miezi miwili ya kwenda, na miezi miwili ya kurudi, lakini pamoja na hayo, Afriti huyo akasema: Mimi ninakuhakikishia kwamba nitakuletea licha ya ukubwa wake na uzito wake na umbali wake, kabla hujainuka kutoka katika baraza lako hili ambalo uko. Na ni desturi kwamba mabaraza marefu huwa katika wakati wa kuanzia kuinuka juu kwa jua asubuhi (dhuhaa) hadi thuluthi moja ya siku. Na huo ndio mwisho wa desturi, na inaweza kuwa chini ya hivyo au zaidi. Na huyu ndiye mfalme mkubwa, ambaye ni mmoja tu wa wale walio chini yake na kiasi hiki cha nguvu na uwezo. Na zaidi ya hilo kwamba "Akasema mwenye elimu ya Kitabu." Wafasiri walisema: ni mwanamume mwema mwenye elimu aliyekuwepo kwa Suleiman, alikuwa anaitwa Asif ibn Barkhia. Alikuwa anajua jina la Mwenyezi Mungu kuu zaidi, ambalo anapoombwa kwalo, anajibu, na alipoulizwa kitu kwalo, anapeana. "Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako" kwa kumuomba kwa kulitaja jina hilo kuu, na papo hapo kinakuja, na kwamba alimuomba Mwenyezi Mungu, nacho kikaja. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi; ikiwa haya ndiyo makusudio yake, au alikuwa na elimu ya Kitabu ambayo kwayo angeweza kuleta yaliyo mbali na kufanikisha magumu? "Basi" Suleiman "alipokiona kimewekwa kimetulia mbele yake," akamsifu Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kumpa uwezo na ufalme, na kumrahisishia mambo yake, na "akasema: Haya ni katika fadhila zake Mola wangu Mlezi, ili anijaribu nitashukuru au nitakufuru," ili anijaribu kwa hayo. Lakini yeye, amani iwe juu yake, hakudanganyika na ufalme wake, na utawala wake, na uwezo wake kama ilivyo desturi ya wafalme wajinga. Badala yake alijua kwamba huu ulikuwa mtihani kutoka kwa Mola wake Mlezi, kwa hivyo akahofia kwamba anaweza kutozishukuru neema hizi, kisha akabainisha kwamba shukrani hii haimfaidi Mwenyezi Mungu kitu, lakini badala yake faida yake inamrudia mwenyewe. Alisema, "Na mwenye kushukuru, kwa hakika, anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake. Na anayekufuru, kwa hakika Mola wangu Mlezi ni Mkwasi na Karimu." Yeye si mhitaji wa matendo yake, ni Karimu mwenye heri nyingi, ambayo anawapia wote; mwenye kushukuru na mwenye kukufuru; isipokuwa kwamba kushukuru neema yake kunamsababishia mtu kuzidishiwa neema zaidi, na kuzikufuru kunasababisha kuondoka kwake.