Ash-Shu'araa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
قَالَ أَفَرَءَيْتُم مَّا كُنتُمْ تَعْبُدُونَ ۷۵ أَنتُمْ وَءَابَآؤُكُمُ ٱلْأَقْدَمُونَ ۷۶ فَإِنَّهُمْ عَدُوٌّ لِّىٓ إِلَّا رَبَّ ٱلْعَـٰلَمِينَ ۷۷ ٱلَّذِى خَلَقَنِى فَهُوَ يَهْدِينِ ۷۸ وَٱلَّذِى هُوَ يُطْعِمُنِى وَيَسْقِينِ ۷۹ وَإِذَا مَرِضْتُ فَهُوَ يَشْفِينِ ۸۰ وَٱلَّذِى يُمِيتُنِى ثُمَّ يُحْيِينِ ۸۱ وَٱلَّذِىٓ أَطْمَعُ أَن يَغْفِرَ لِى خَطِيٓـَٔتِى يَوْمَ ٱلدِّينِ ۸۲
{75-82} Ibrahimu akawaambia, "Nyinyi na baba zenu nyote ni wapinzani katika jambo hili, na maneno kwao wote ni mamoja: "Je, mmewaona hawa mnaowaabudu? Nyinyi na baba zenu wa zamani? Kwani hakika hao ni adui zangu." Basi na wajaribu kunidhuru kwa madhara hata kidogo, na wanifanyie njama, lakini hawataweza; "isipokuwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. Ambaye ndiye aliyeniumba, na Yeye ndiye ananiongoa." Yeye tu ndiye wa pekee katika neema ya uumbaji na neema ya kuongoza kwenye masilahi ya kidini na ya kidunia, na kisha akatenga baadhi ya mahitaji hayo, akasema, "Na ambaye ndiye ananilisha na kuninywesha. Na ninapougua, ni Yeye ndiye anayeniponesha. Na ambaye atanifisha, na kisha atanihuisha. Na ambaye ndiye ninayemtumai kunisamehe makosa yangu Siku ya Malipo." Huyu ndiye peke yake anayeweza kufanya hayo, kwa hivyo ni lazima aabudiwe Yeye peke yake na atiiwe, na yaachwe masanamu haya ambayo hayaumbi wala hayaongoi, wala hayauguzi wala hayaponyi, wala hayalishi wala hayanyweshi, wala hayafishi wala hayahuishi, wala hayawanufaishi wale wanaoyaabudu kwa kuwaondolewa taaba, wala kuwasamehe dhambi. Basi huu ni ushahidi wa kukata na hoja yenye kug'aa ambayo nyinyi wala baba zenu hamuwezi kuipinga, kwa hivyo hilo likaonyesha kwamba mnashirikiana katika upotovu na kuiacha njia ya uwongofu na unyoofu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na kaumu yake wakamhoji. Akasema: Je, mnanihoji juu ya Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ameniongoa..." hadi mwisho wa Aya hizi.