Ash-Shu'araa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
قَالَ رَبُّكُمْ وَرَبُّ ءَابَآئِكُمُ ٱلْأَوَّلِينَ ۲۶ قَالَ إِنَّ رَسُولَكُمُ ٱلَّذِىٓ أُرْسِلَ إِلَيْكُمْ لَمَجْنُونٌ ۲۷
{26-27} Kwa hivyo, Musa akasema, "Ndiye Mola wenu Mlezi, na Mola Mlezi wa baba zenu wa kwanza." Mustaajabu au la, mfanye kiburi au mtii. Kwa hivyo Firauni akasema kwa kupinga haki na kumtia doa yule aliyekuja nayo, "Hakika huyu Mtume wenu aliyetumwa kwenu ni mwendawazimu." Ambapo alisema kinyume na yale tulivyo nayo, na akatuhalifu kwa tunavyoamini. Kwa hivyo, akaona kwamba kulingana na yeye na wale wenye akili, ni kwamba wenye akili ni wale wanaodai kwamba hawakuumbwa, au kwamba mbingu na ardhi ziliendelea kuwepo bila kuumbwa, na kwamba wao wenyewe waliumbwa bila muumba! Na kulingana na yeye ni kwamba, akili bora ni kwamba aabudiwe kiumbe mpungufu katika namna zote! Na wazimu kulingana na yeye ni kuthibitisha kuwepo Mola Mlezi, Muumba wa ulimwengu wa juu na wa chini, ambaye ameneemesha kwa neema za dhahiri na za ndani, na kwamba abudiwe! Naye aliwapambia kaumu yake auli hii, nao walikuwa wapumbavu wenye akili ndogo. "Basi akawachezea kaumu yake, nao wakamtii. Kwa hakika, hao walikuwa kaumu wapotovu."