Ash-Shu'araa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
ٱلَّذِى يَرَىٰكَ حِينَ تَقُومُ ۲۱۸ وَتَقَلُّبَكَ فِى ٱلسَّـٰجِدِينَ ۲۱۹ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ ۲۲۰
{218 - 220} Kisha akatanabahisha juu ya kutafuta msaada kwa kutambua ukaribu wa Mwenyezi Mungu na kushuka katika mahali pa ihsani. Akasema, "Ambaye anakuona unaposimama. Na mageuko yako kati ya wanaosujudu." Yaani, anakuona katika ibada hii kuu, ambayo ni swala, wakati unapokuwa umesimama, na mageuko yako ukirukuu na kusujudu. Na aliyataja haya haswa kwa sababu ya ubora wake na utukufu wake, na kwa sababu mwenye kuhisi ndani yake ukaribu wa Mola wake Mlezi; anajinyenyekeza, na kujidhalilisha, na kuikamilisha, na kwa kuikamilisha yanakamilika matendo yake mengineyo yote, na anatafuta msaada wa hayo katika mambo yake yote. "Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia" sauti zote pamoja na utofauti wake, na wingi wake, na aina zake mbalimbali. "Mwenye kujua zaidi" ambaye anajua vilivyo ya dhahiri na vya ndani, na ghaibu na yanayoonekana. Kwa hivyo, ikiwa mja atahisi kwamba Mwenyezi Mungu anamuona katika hali zake zote, na kwamba anamsikia anayosema, na kwamba anajua yaliyo moyoni mwake ya wasiwasi kubwa, na azimio, na nia mbalimbali ni katika mambo yenye kumsaidia kufikia daraja ya ihsani.