پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Ash-Shu'araa
سورهٔ ۲۶

Ash-Shu'araa

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۲۱۵

وَٱخْفِضْ جَنَاحَكَ لِمَنِ ٱتَّبَعَكَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ ۲۱۵

{215} "Na watwae kwa upole wanaokufuata miongoni mwa Waumini." Kwa ulaini, na upole katika kuwaongelesha, na kuwapenda, na kuwaonyesha tabia nzuri, na kuwafanyia hisani kamili. Naye Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alikwisha fanya hivyo, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio umekuwa laini kwao. Na lau ungelikuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangelikukimbia. Basi wasamehe, na waombee maghfira, na shauriana nao katika mambo." Na hizi ndizo tabia zake - yeye rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ambazo ni tabia kamilifu zaidi, ambazo kwazo mtu anapata masilahi makubwa na anazuilika na madhara kama inavyoshuhudiwa. Basi je, inafaa kwa yule anayemuamini Mwenyezi Mungu na Mutume wake anayedai kumfuata na kumuiga kuwa kwamba yeye ndiye mzigo kwa Waislamu, muovu wa maadili, mkali na mgumu wa moyo juu yao. Na akiwaona wakiasi au tabia mbaya, anawagura, na kuwachukia, hana ulaini wowote kwao wala tabia nzuri, wala kuunganisha watu. Yaliyotokea yaliyotokea kwa sababu ya haya yenye uharibifu na kupoteza masilahi, lakini pamoja na hayo, utamkuta anamdharau yule ambaye anasifika kwa sifa za Mtume mtukufu, huku anashutumu kwa unafiki na kwamba anasalimu amri kwa maadui. Kisha akajitaja yeye mwenyewe na akajiinua juu na akapendezwa na matendo yake? Basi je, hayo si isipokuwa kwa sababu ya ujinga wake na kupambiwa hayo na kuhadaiwa na Shetani?!