Ash-Shu'araa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
كَذَّبَتْ قَوْمُ نُوحٍ ٱلْمُرْسَلِينَ ۱۰۵ إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ نُوحٌ أَلَا تَتَّقُونَ ۱۰۶ إِنِّى لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ ۱۰۷ فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ ۱۰۸ وَمَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ ۱۰۹ فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ ۱۱۰
{105-110} Yeye Mtukufu anataja kukadhibisha kwa kaumu ya Nuhu Mtume wao Nuhu, na kile alichowajibu na kile walichomjibu, na adhabu yao wote. Akasema, "Kaumu ya Nuhu waliwakadhibisha Mitume" wote, kwa sababu kumkadhibisha Nuhu ni kama kuwakadhibisha Mitume wote; kwa sababu wote walikubaliana juu ya wito mmoja na habari moja; kwa hivyo kumkadhibisha mmoja wao tu, ni kama kukadhibisha haki waliyokuja nayo wote. Walimkadhibisha, "Alipowaambia ndugu yao" katika nasaba "Nuhu." Na Mwenyezi Mungu aliwatuma Mitume kutoka katika nasaba ya wale aliowatumia Mtume huyo; ili wasije wakachukizwa na kumtii asiyetoka katika wao, na kwa sababu wanajua uhakika wake; na hawahitaji kumchnguza. Basi akawaambia kwa maneno ya upole zaidi kama ilivyo njia ya Mitume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, "Je, hamchi Mwenyezi Mungu" Mtukufu, mkaacha kile mnachodumu kukiabudu cha masanamu, na mkamfanyia Mwenyezi Mungu peke yake ibada? "Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu" Na kwa kuwa yeye ni Mtume mahususi kwao, inalazimu wapokee kile alichotumwa nacho kwao, na kukiamini, na wamshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuwatumia wao tu Mtume huyu mtukufu. Na kwa kuwa yeye ni mwaminifu inalazimu kwamba asiongee juu ya Mwenyezi Mungu, asiongeze katika Ufunuo wake, na asipunguze kitu. Na hayo yanalazimu wazisadiki habari zake na watii amri zake. "Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nitiini mimi" katika yale aliyowaamrisha na katika yale aliyowakataza. Kwa maana hayo ndiyo yanayotokana na yeye kuwa ni Mtume mwaminifu kwao. Na ndiyo maana akatumia baada yake "basi" inayoonyesha sababu ya kuwaamrisha wamche. Kwa hivyo akawa ametaja sababu inayolazimu wamche, kisha akataja kwamba hakuna kizuizi chochote dhidi ya hilo. Akasema, "Na siwaulizi juu yake ujira" ndiyo mkaona ugumu wa gharama hiyo nzito. "Kwani ujira wangu hauko isipokuwa kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote." Ninatumaini kuwa karibu naye kwa hilo, na thawabu nyingi. Na ama nyinyi matamanio yangu na mwisho wa utashi wangu kwenu ni kuwashauri na kwamba mfuate njia iliyonyooka. "Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nitiini mimi." Alirudia hilo yeye amani iwe juu yake kwa sababu alirudiarudia kuwalingania watu wake na akakaa muda mrefu katika kufanya hivyo, kama alivyosema Yeye Mtukufu, "na akakaa nao miaka elfu kasoro miaka hamsini." Na "Akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimewalingania watu wangu usiku na mchana. Lakini wito wangu haukuwazidisha ila kukimbia..." hadi mwisho wa Aya hizi.