Al-Furqaan
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَلَقَدْ ءَاتَيْنَا مُوسَى ٱلْكِتَـٰبَ وَجَعَلْنَا مَعَهُۥٓ أَخَاهُ هَـٰرُونَ وَزِيرًا ۳۵ فَقُلْنَا ٱذْهَبَآ إِلَى ٱلْقَوْمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا فَدَمَّرْنَـٰهُمْ تَدْمِيرًا ۳۶ وَقَوْمَ نُوحٍ لَّمَّا كَذَّبُوا۟ ٱلرُّسُلَ أَغْرَقْنَـٰهُمْ وَجَعَلْنَـٰهُمْ لِلنَّاسِ ءَايَةً ۖ وَأَعْتَدْنَا لِلظَّـٰلِمِينَ عَذَابًا أَلِيمًا ۳۷ وَعَادًا وَثَمُودَا۟ وَأَصْحَـٰبَ ٱلرَّسِّ وَقُرُونًۢا بَيْنَ ذَٰلِكَ كَثِيرًا ۳۸ وَكُلًّا ضَرَبْنَا لَهُ ٱلْأَمْثَـٰلَ ۖ وَكُلًّا تَبَّرْنَا تَتْبِيرًا ۳۹ وَلَقَدْ أَتَوْا۟ عَلَى ٱلْقَرْيَةِ ٱلَّتِىٓ أُمْطِرَتْ مَطَرَ ٱلسَّوْءِ ۚ أَفَلَمْ يَكُونُوا۟ يَرَوْنَهَا ۚ بَلْ كَانُوا۟ لَا يَرْجُونَ نُشُورًا ۴۰
{35-40} Mwenyezi Mungu Mtukufu aliviashiria visa hivi, na alikwisha vieleza kwa kina katika aya nyinginezo; ili wale wanaoongeleshwa wajitahadhari dhidi ya kuendelea kumkadhibisha Mtume wao, wakaja fikwa na yale yaliyowafika umma ambao walikuwa karibu nao, na ambao wanajua visa vyao kutoka kwa habari zilizoenea na ambazo ni mashuhuri kuhusiana nao. Na hata tena kuna wale ambao wanaona athari zao kwa macho, kama vile kaumu ya Swalih wa huko Al-Hijr, na mji ambao ulinyeshewa mvua mbaya ya mawe ya udongo wa Motoni. Wakawa wanawapitia wakati wa asubuhi, na usiku katika safari zao. Umma hao sio waovu zaidi yao, na Mitume wao sio bora zaidi kuliko Mtume wa hawa. "Je, makafiri wenu ni bora kuliko hao, au yameandikwa vitabuni kuwa nyinyi hamtiwi makosani?" Lakini kile kilichowazuia hawa kuamini pamoja na kile walichokiona miongoni mwa Ishara mbalimbali ni kwamba hawakuwa wanatarajia kufufufuka au kutawanywa kutoka makaburini mwao. Kwa hivyo hawatumaini kukutana na Mola wao Mlezi, wala hawahofu adhabu yake. Na ndiyo maana wakaendelea na ukaidi wao. Vinginevyo, tayari zilikwisha wajia ishara ambazo haiwezi kubakia pamoja nazo shaka yoyote wala fikira potovu, wala shida wala hata kusitasita.