پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Furqaan
سورهٔ ۲۵

Al-Furqaan

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیه‌های ۲۵–۲۶

وَيَوْمَ تَشَقَّقُ ٱلسَّمَآءُ بِٱلْغَمَـٰمِ وَنُزِّلَ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ تَنزِيلًا ۲۵ ٱلْمُلْكُ يَوْمَئِذٍ ٱلْحَقُّ لِلرَّحْمَـٰنِ ۚ وَكَانَ يَوْمًا عَلَى ٱلْكَـٰفِرِينَ عَسِيرًا ۲۶

{25-26} Yeye Mtukufu anajulisha juu ya ukuu wa Siku ya Qiyama na magumu, na shida na mambo yatakayoisumbua mioyo ndani yake. Akasema, "Na siku zitakapopasuka mbingu zifunguke kwa mawingu," na wingu hilo ndilo atakaloteremka Mwenyezi Mungu ndani yake. Atashuka kutoka mbinguni, kwa hivyo zivunike mbingu kwa sababu ya hilo, na zipasuke, na washuke [Malaika] wa kila mbingu, kisha wasimame safu kwa safu. Ima safu moja yenye kuwazunguka viumbe vyote, au Malaika wa kila mbingu watakuwa katika safu, kisha wa mbingu inayofuata katika safu, vivyo hivyo. Na makusudio ni kwamba Malaika pamoja na wingi wao na nguvu zao watashuka wawazunguke viumbe, nao wataidhalilikia amri ya Mola wao Mlezi, na hakuna hata mmoja wao atakayezungumza isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Basi unafikiriaje juu ya mwanadamu dhaifu, haswa yule aliyesimama kidete dhidi ya Mmiliki wake kwa madhambi makuu, na akafanya anayochukia, kisha akamjia na dhambi na makosa ambayo hakuyatubia. Kisha Mfalme, Muumba vyote atahukumu kwa hukumu ambayo haina ukandamizaji wowote wala dhuluma hata uzito wa chembe. Na ndiyo maana, akasema, "Na itakuwa siku ngumu kwa makafiri," kwa sababu ya ugumu wake mkubwa, na mambo yake kumuwia magumu. Tofauti na Muumini, mambo yake tayamuwia mepesi na rahisi kuyabeba. "Siku tutakayowakusanya wachamungu kuwapeleka kwa Arrahmani (Mwingi wa rehema) kuwa ni wageni wake." "Na tukawaswaga wahalifu kwenda katika Jahannamu hali ya kuwa wana kiu." Na kauli yake, "Ufalme wa haki siku hiyo" ya Qiyama "utakuwa wa Arrahman (Mwingi wa rehema)." Yaani, hakuna hata mmoja wa viumbe atakayebakia na ufalme au hata mfano wa ufalme kama walivyokuwa katika dunia. Bali wafalme na raia watakuwa sawa, watu huru na watumwa, wakuu na wengineo. Na katika yale yanayoufanya moyo kupumzika, na nafsi kutulia, na kifua kupanuka ni kwamba aliufungamanisha ufalme wa Siku ya Qiyama na jina lake Mwingi wa rehema, ambaye rehema yake ilikienea kila kitu, na kukijumuisha kila kilicho hai, na kuvijaa viumbe, na akaijumuisha dunia na Akhera kwa hiyo. Na kwayo kikamilika kila kilicho kipungufu, na kwayo ukaondoa kila upungufu, na majina yanayoiashiria yalishinda yale yenye kuashiria ghadhabu yake, na rehema yake ilitangulia ghadhabu yake na kuishinda. Na akamuumba mwanadamu huyu dhaifu na kumpa heshima na kumtukuza ili amtimizie neema yake na kumfunika kwa rehema yake. Nao watakuwa wamehudhuria katika mahali penye udhalilifu, unyenyekevu, na kutokuwa na kiburi mbele yake. Wakawa wanangojea kile atakachohukumu kuhusiana nao na kile atakachowafanyia. Naye ni mwenye kuwarehemu zaidi hata kuliko wao wenyewe na wazazi wao. Basi unafikiri ataamilianaje nao. Na wala haangamii mbele ya Mwenyezi Mungu isipokuwa mwenye kuangamia. Na wala hatoki katika rehema yake isipokuwa yule ambaye yu mashakani mno, aliyestahiki neno la adhabu.