Taa-Haa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
إِنَّنِىٓ أَنَا ٱللَّهُ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّآ أَنَا۠ فَٱعْبُدْنِى وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ لِذِكْرِىٓ ۱۴
{14} Kisha akaeleza aliyomteremshia kwa kauli yake, ''Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu. Hapana mungu isipokuwa Mimi tu." Mwenyezi Mungu ambaye anastahiki uungu, mwenye kusifika kwa huo. Kwa sababu Yeye ndiye mkamilifu katika majina yake na sifa zake, wa pekee katika vitendo vyake, ambaye hana mshirika yeyote, wala anayefanana naye, wala anayelingana naye, wala aliye sawa naye. "Basi niabudu Mimi" kwa aina zote za ibada, za nje na za ndani, za msingi na matawi. Kisha akaitaja swala kwa namna maalumu, hata ingawa inaingia katika ibada, kwa sababu ya fadhila zake, na utukufu wake, na kujumuisha kwake uja wa kimoyo, ulimi, na viungo. Na kauli yake, "kwa ajili ya kunikumbuka Mimi" kwa sababu kumdhukuru Yeye Mtukufu ndilo lengo kubwa zaidi, na kwa hilo ndiyo unakuwa uja wa moyo, na kwa hilo ndiyo unapata furaha. Na moyo ambao haumkumbuki Mwenyezi Mungu, hauwezi kufikia heri yoyote na umeharibika kuharibika kwote. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akawawekea waja wake sheria ya aina mbalimbali za ibada ambazo zimekusudiwa kwazo kusimamisha utajo wake, hasa swala. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema, ''Soma yale uliyofunuliwa katika Kitabu, na ushike Swala. Hakika Swala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumtaja Mwenyezi Mungu ndilo jambo kubwa kabisa.'' Yaani, yaliyomo humo ya utajo wa Mwenyezi Mungu ndiyo makubwa zaidi hata kuliko yale ya kukataza machafu na maovu. Na hayo ya utajo wa Mwenyezi Mungu ndiyo huitwa: Kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika ibada. Kwa maana, uungu ni sifa yake Yeye Mtukufu, na uja ni sifa ya mja wake.