Al-Baqara
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَقَالُوا۟ لَن تَمَسَّنَا ٱلنَّارُ إِلَّآ أَيَّامًا مَّعْدُودَةً ۚ قُلْ أَتَّخَذْتُمْ عِندَ ٱللَّهِ عَهْدًا فَلَن يُخْلِفَ ٱللَّهُ عَهْدَهُۥٓ ۖ أَمْ تَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ۸۰
(80) Alitaja matendo yao maovu, kisha akataja - pamoja na hayo - kwamba wao wanazitakasa nafsi zao, na kwamba wanajishuhudia kwamba wataepukana na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na watapata malipo yake mazuri. Na kwamba hawataguswa na Moto ila siku chache zinazohesabika kwa vidole. Kwa hivyo, wakawa wamekusanya kati ya kuasi na amani. Na pindi yalipokuwa haya ni madai tu, Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwajibu, akasema "Sema" uwaambie ewe Mtume "Je, mmechukua ahadi kwa Mwenyezi Mungu?” Yani kwa kumuamini Yeye na Mitume wake na kumtii. Na hii ndiyo ahadi yenye kumwokoa mtu wake (mwenye kuchukua ahadi), ambayo haibadiliki wala haigeuki. "Au mnasema juu ya Mwenyezi Mungu mambo msiyoyajua?" Basi (Mwenyezi Mungu) Mtukufu akatoa habari kwamba ukweli wa madai yao unategemea moja ya mambo haya mawili, ambayo hayana la tatu. Ima wawe walichukua ahadi kwa Mwenyezi Mungu; kwa hivyo madai yao yakawa ni sahihi. Na ima wawe wanamsingizia; basi yakawa ya uongo, kwa hivyo ikawa inafaa zaidi kuwapa hizaya na kuwaadhibu. Na imekwisha julikana katika hali yao kwamba, hawakuchukua ahadi na Mwenyezi Mungu kwa sababu ya kukadhibisha kwao wengi wa Manabii, mpaka hali ikawafikia kiwango kwamba waliua kundi miongoni mwao, na kwa kukataa kwao kumtii Mwenyezi Mungu na kuvunja kwao maagano. Basi ikawa wazi kwa hilo kwamba wanamsingizia na kumzulia tu yale wasiyoyajua? Na kumzungumizia (Mwenyezi Mungu) bila ya elimu ni katika haramu kubwa mno na mambo mabaya ya kuchukiza zaidi.