پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
سورهٔ ۲

Al-Baqara

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۴۰

يَـٰبَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ ٱذْكُرُوا۟ نِعْمَتِىَ ٱلَّتِىٓ أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَوْفُوا۟ بِعَهْدِىٓ أُوفِ بِعَهْدِكُمْ وَإِيَّـٰىَ فَٱرْهَبُونِ ۴۰

Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akaanza kuwakumbusha Wana wa Israili neema zake juu yao na ihsani yake, akasema:

(40) “Enyi Wana wa Israili!” Anayekusudiwa na Israili ni Yaaqub, amani iwe juu yake. Na haya maneno ni kwa makundi ya Wana wa Israili waliokuweko huko Madina na pembezoni mwake. Na wanaingia ndani yao waliokuja baada yao. Basi akawaamrisha amri ya jumla, akasema: “Kumbukeni neema yangu niliyokuneemesheni.” Nayo inajumuisha neema zote ambazo baadhi yake zitatajwa katika sura hii. Na kinachokusudiwa ni kuzitaja kwa moyo ili kuzikubali, na kwa ulimi ili kuzisifu, na kwa viungo kwa kuzitumia katika yale anayoyapenda na kuyaridhia. “Na timizeni ahadi yangu,” nayo ni yale aliyowaagiza kama vile kumuamini Yeye na Mitume wake na kusimamisha Sheria yake. “Na Mimi nitatimiza ahadi yenu,” nayo ni malipo kwa hayo. Na makusudio ya hilo ni yale aliyoyataja Mwenyezi Mungu katika kauli yake: “Na Mwenyezi Mungu alichukua agano la Wana wa Israili. Na tukawateulia kutokana nao wakuu kumi na wawili. Na Mwenyezi Mungu akasema: Kwa yakini Mimi ni pamoja nanyi. Mkisali, na mkatoa Zaka, na mkawaamini Mitume wangu;” hadi kauli yake “bila ya shaka atakuwa amepotea njia iliyo sawa.” Kisha akawaamrisha sababu itakayowafanya kutimiza agano lake, nayo ni kumhofu yeye Mtukufu, na kumnyenyekea yeye peke yake. Kwa sababu mwenye kumnyenyekea, huko kunyenyekea kwake kutamfanya kutekeleza amri yake na kuepukana na makatazo yake. Kisha akawaamrisha amri maalumu, ambayo haitimii imani yao wala haikubaliki isipokuwa kwayo, akasema: