Al-Baqara
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ وَأَقَامُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُا۟ ٱلزَّكَوٰةَ لَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ۲۷۷ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَذَرُوا۟ مَا بَقِىَ مِنَ ٱلرِّبَوٰٓا۟ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ۲۷۸ فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا۟ فَأْذَنُوا۟ بِحَرْبٍ مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ ۖ وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَٰلِكُمْ لَا تَظْلِمُونَ وَلَا تُظْلَمُونَ ۲۷۹
{277 - 279} "Hakika, wale walioamini na wakatenda mema na wakashika Swala na wakatoa Zaka." Aya hii ni kwa ajili ya kubainisha kuwa kubwa zaidi ya sababu za kujiepusha na yale aliyoharamisha Mwenyezi Mungu katika mapato yenye riba ni kuikamilisha imani na haki zake, hasa kushika swala na kutoa zaka. Kwa sababu, swala inakataza machafu na maovu. Nayo Zaka ambayo ni kuwafanyia viumbe wema inapingana na riba ambayo ni kuwadhulumu na kuwafanyia ubaya. Kisha akaelekeza mazungumzo kwa Waumini, na akawaamrisha kuiogopa (riba), na waache yale yaliyobaki katika mapatano ya riba ambayo walikuwa wakiyafanya kabla ya hapo. Na kwamba wasipofanya hivyo, basi wao wanapigana vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na hili ni katika makubwa mno yanayoonyesha ubaya wa riba, kwani alimfanya mwenye kuendelea kuifanya kuwa anapigana vita dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kisha akasema, "na mkitubu" yani kutokana na miamala ya riba "basi haki yenu ni rasilimali zenu. Msidhulumu" watu kwa kuchukua riba "wala msidhulumiwe" kwa kupunguziwa mtaji wenu. Kwa hivyo, kila mwenye kutubia kutokana na riba, ikiwa ni miamala iliyopita, basi ni chake kilichopita, na jambo lake litachunguzwa. Na ikiwa ni miamila iliyopo basi inamlazimu kuchukua mtaji wake peke yake. Na ikichukua ziada, basi atakuwa ameifanyia riba ujasiri. Na katika Aya hii, kuna ubainisho wa hekima ya riba, na kwamba ni inajumuisha kuwadhulumu wenye mahitaji kwa kuchukua ziada na kuwazidishia riba, ingawa ni wajibu kuwapa muda. Na kwa sababu hii, akasema: