Al-Baqara
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَٰلَهُم بِٱلَّيْلِ وَٱلنَّهَارِ سِرًّا وَعَلَانِيَةً فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ۲۷۴
{274} "Wale wanaotoa mali zao usiku na mchana, kwa siri na dhahiri, wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi; wala haitakuwa hofu juu yao, wala wao hawatahuzunika." Mwenyezi Mungu atawatia katika kivuli chake siku ambayo hakutakuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake. Na Mwenyezi Mungu atawapa mema na kuwazuia huzuni, hofu na machukizo. Na kauli yake, "wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi." Yani kila mmoja wao kulingana na hali yake. Na kusema kwamba hilo liko hususan kwa Mola wao Mlezi kunaashiria utukufu wa hali hii, na kufikia kwake katika nafasi kubwa zaidi, kama ilivyo katika hadithi sahihi: “Hakika, mja anaweza toa sadaka ya tende kutoka katika kuchuma kuzuri, kwa hivyo Al-Jabbar (Afanyaye atakalo) anaikubali kwa mkono wake. Kisha akaikuzia mmoja wenu, kama vile mmoja wenu anavyomkuza mwana farasi wake aliyemwachisha kunyonya mpaka awe mfano wa mlima mkubwa.”