پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
سورهٔ ۲

Al-Baqara

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۲۵۸

أَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِى حَآجَّ إِبْرَٰهِـۧمَ فِى رَبِّهِۦٓ أَنْ ءَاتَىٰهُ ٱللَّهُ ٱلْمُلْكَ إِذْ قَالَ إِبْرَٰهِـۧمُ رَبِّىَ ٱلَّذِى يُحْىِۦ وَيُمِيتُ قَالَ أَنَا۠ أُحْىِۦ وَأُمِيتُ ۖ قَالَ إِبْرَٰهِـۧمُ فَإِنَّ ٱللَّهَ يَأْتِى بِٱلشَّمْسِ مِنَ ٱلْمَشْرِقِ فَأْتِ بِهَا مِنَ ٱلْمَغْرِبِ فَبُهِتَ ٱلَّذِى كَفَرَ ۗ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ ۲۵۸

{258} Mwenyezi Mungu anatuhadithia katika habari za Mitume na wale waliotangulia ambazo hakika zinabainika kwazo, na hoja mbalimbali zinasimama juu ya Tauhidi. Basi Mola Mtukufu akajulisha kuhusu rafiki mwandani wake Ibrahim – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake wakati alipomhoji mfalme huyu mkandamizaji. Ambaye ni Namrud wa Babeli, aliyemkanusha na kumkataa Mola Mlezi wa walimwengu wote. Na akajitoa kumpinga Ibrahim Al-Khalil na kuhojiana naye katika jambo hili ambalo halikubali shaka yoyote, wala tatizo, wala shaka. Na ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu na umola wake ambao ndiyo mambo yaliyo wazi kabisa na yaliyo dhahiri zaidi. Lakini mkandamizaji huyu alidanganywa na ufalme wake, na ukamfanya kupindukia mpaka hali ikamfikisha kwamba alimkataa (Mwenyezi Mungu). Na akahojiana na Ibrahim Mtume mtukufu ambaye Mwenyezi Mungu alimpa elimu na yakini. Ambavyo hakumpa yeyote katika Mitume isipokuwa Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Ibrahim akasema akihojiana naye, “Mola wangu Mlezi ndiye anayehuisha na anayefisha.” Yani Yeye ndiye pekee yake mwenye kuumba, kuendesha mambo, kuhuisha na kufisha. Kwa hivyo akataja katika aina hii kile cha dhahiri mno, ambacho kuhuisha na kufisha. Hivyo, mkandamizaji huyu akasema akijifahirisha, “mimi pia ninahuisha na ninafisha.” Na akamaanisha kwa hilo kuwa ninamuua nitakaye kumuua na ninamwacha hai ninayetaka kumuacha. Na Inavyojulikana ni kwamba huku ni kuficha na kupotosha kando na kilichokusudiwa. Na kwamba kilichokusudiwa ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye wa pekee katika kuleta uhai katika mambo yasiyokuwapo na kuurejesha kwa wafu. Na kwamba Yeye ndiye anayewafisha waja na wanyama kwa mida yao kwa sababu alizofungamanisha na hilo, na bila ya sababu. Basi Al-Khalil alipomwona akificha kuficha ambako huenda ukaenea miongoni mwa watu wa kawaida, Ibrahim akasema kwa kumlazimisha kusadikisha kauli yake ikiwa ni kama anavyodai. “Kwa hakika, Mwenyezi Mungu hulileta jua kutokea mashariki, basi wewe lilete kutokea magharibi. Kwa hivyo, akashindwa yule aliyekufuru.” Yani alisimama na hoja yake ikakatika, na fikira yake potofu ikatoweka. Na hili kutoka kwa Al-Khalil sio kuhama kutoka kwa ushahidi mmoja hadi ushahidi mwingine. Bali ni kumlazimu Namrud kuendelea kuthibitisha ushahidi wake ikiwa yeye ni mkweli. Na alitumia ushahidi huu ambao haukubali kuenezwa, wala kughushi, na wala kufichwa. Kwa hivyo ushahidi wote wa kusikia, wa kiakili na wa umbile la asili (wa kuzaliwa) wote ulikwisha simama kama shahidi juu ya upweke wa Mwenyezi Mungu. Ukikubali upweke wake katika kuumba, kuendesha mambo, na kwamba yule ambaye jambo lake ni hili, basi haistahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye tu. Na Mitume wote wanaafikiana juu ya msingi huu mkubwa, na wala hakuwahi kuupinga isipokuwa mkaidi, mwenye kiburi mfano wa mkandamizaji huyu mkaidi. Basi hizi ni katika dalili za Tauhidi. Kisha akataja dalili za ukamilifu wa uwezo, na ufufuo, na malipo. Akasema: