Al-Baqara
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
ٱلطَّلَـٰقُ مَرَّتَانِ ۖ فَإِمْسَاكٌۢ بِمَعْرُوفٍ أَوْ تَسْرِيحٌۢ بِإِحْسَـٰنٍ ۗ وَلَا يَحِلُّ لَكُمْ أَن تَأْخُذُوا۟ مِمَّآ ءَاتَيْتُمُوهُنَّ شَيْـًٔا إِلَّآ أَن يَخَافَآ أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ ٱللَّهِ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ ٱللَّهِ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا فِيمَا ٱفْتَدَتْ بِهِۦ ۗ تِلْكَ حُدُودُ ٱللَّهِ فَلَا تَعْتَدُوهَا ۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ ٱللَّهِ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ ۲۲۹
{229} Talaka ilikuwa katika Jahiliyya, na ikaendelea hivyo mwanzo wa Uislamu. Mwanamume alikuwa akimtaliki mkewe bila ya kuwepo na kikomo (cha talaka hizo). Kwa hivyo, alikuwa anapotaka kumdhuru (mkewe), alimpa talaka, na anapokaribia kumaliza eda yake, anamrejesha. Kisha anamtaliki, na anamfanyia vivyo hivyo milele, kwa hivyo anapata kutokana na hilo madhara ambayo Mwenyezi Mungu ndiye anayeyajua tu. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akasema kwamba, "talaka" ambayo mume anaweza kumrejesha mkewe, "ni mara mbili." Ili ikiwa mume hakukusudia kumdhuru, ataweza kumrejesha na kufikiria tena katika kipindi hiki. Lakini jambo lolote zaidi ya hilo, basi hilo halifai. Kwa sababu, mwenye kufanya hivyo zaidi ya mara mbili, ima anatafuta la haramu au hataki kuendelea kukaa naye. Bali lengo lake ni kumdhuru. Ndiyo maana Mola Mtukufu akamwamrisha mume akae na mkewe "kwa wema." Yani aishi naye kwa wema mfano wa wanavyowafanyia wenzake wake zao. Na hii ndiyo rai sahihi zaidi. La sivyo, amwachilie na aachane naye "kwa uzuri". Na katika uzuri, ni kwamba (mume) asichukue wakati wa kuachana naye chochote katika mali ya mkewe. Kwa sababu, hiyo ni dhuluma, na kachukua mali bila ya malipo yoyote. Na ndio maana akasema: "Wala si halali kwenu kuchukua chochote katika kile mlichowapa wake zenu, isipokuwa ikiwa wote wawili watahofia kwamba hawataweza kushikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu." Na hii ndiyo Mukhala' (yani mke kujinunua) kwa wema, ikiwa mke atamchukia mumewe kwa sababu ya maadili yake au maumbile yake au upungufu katika dini yake. Na akaogopa kwamba hatamtii Mwenyezi Mungu katika huyu mumuwe. "Basi mkihofia kwamba hawataweza kushikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu, hapo hakuna ubaya juu yao katika kile ambacho mke atajikomboa kwacho." Kwa sababu ndicho kibadala cha yeye kufikia lengo lake la kuachana naye. Na katika hili kuna kuwekwa kwa sheria ya khulu ikiwa hekima hii itapatikana. "Hii," yani hukumu kisheria zilizotangulia "ni mipaka ya Mwenyezi Mungu." Yani hukumu zake ambazo aliziweka kama sheria kwenu, na akawaamrisha kusimama nazo. "Na mwenye kuruka mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhalimu." Na ni dhuluma gani iliyo kubwa zaidi kuliko yule aliyeingia ndani ya halali, kisha akaivuka na kuiendea haramu, na kutotosheka na kile ambacho Mungu amekihalalisha? Na dhuluma ni aina tatu: Dhuluma ya mja katika yale yaliyo kati yake na Mwenyezi Mungu. Na dhuluma kubwa ya mja, ambayo ni shirki. Na dhuluma ya mja katika yale yaliyo kati yake na viumbe. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu haisamehei shirki isipokuwa kwa toba. Na haki za waja, Mwenyezi Mungu haachi chochote katika hizo. Na dhuluma ambayo ipo baina ya mja na Mola wake katika yale yaliyo chini ya shirki yapo chini ya mapenzi na hekima ya Mwenyezi Mungu.