Al-Baqara
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَا وَيَسْخَرُونَ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ۘ وَٱلَّذِينَ ٱتَّقَوْا۟ فَوْقَهُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۗ وَٱللَّهُ يَرْزُقُ مَن يَشَآءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ۲۱۲
Mola Mtukufu anajulisha kwamba wale wanaomkufuru Mwenyezi Mungu, na ishara zake na Mitume wake. Na wala hawakuifuata sheria yake, kwamba wamepambiwa maisha ya duniani. Imepambwa kwao katika macho yao na nyoyo zao, na wakayaridhia, na wakatulia nayo, na matamanio yao, mapenzi yao, na matendo yao vikawa vyote kwa ajili yake. Kwa hivyo, wakavielekea, na wakazama katika kuutafuta, na wakautukuza, na wakamtukuza mwenye kushirikiana nao katika hicho kitendo chao. Na wakawadharau Waumini na wakawafanyia masihara, na wakasema: Je, hawa ndio Mwenyezi Mungu aliwafadhilisha miongoni mwetu? Na hili ni kwa sababu ya udhaifu wa akili zao, na uoni wao mfupi. Kwani dunia ni nyumba ya majaribio na mitihani, na zitawapata humo taabu watu wa imani na wa ukafiri. Lakini Muumini hapa duniani hata kama atapatwa na jambo la kuchukiza, yeye atavumilia na kutarajia malipo kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu anampunguzia kwa imani yake na subira yake jambo ambalo haliwi kwa asiyekuwa yeye. Bali jambo zima na mapendeleo ya kweli ni katika nyumba yenye kudumu. Ndio maana Yeye Mtukufu akasema “Na wale wanaomcha Mwenyezi Mungu watakuwa juu yao Siku ya Kiyama.” Basi wachamungu watakuwa katika daraja za juu, wakifurahia kila aina ya neema na furaha, shangwe na nderemo. Na makafiri watakuwa chini yao katika daraja za chini kabisa, wakiadhibiwa kwa kila aina ya adhabu, na kudunishwa, na taabu ya milele isiyo na mwisho. Hivyo basi, katika Aya hii kuna kuwafariji Waumini, na maombolezo kwa makafiri. Na kwa kuwa riziki ya kidunia na ya kiakhera haziwezi kupatikana isipokuwa kwa makadirio ya Mwenyezi Mungu, na hazipatikani isipokuwa kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, yeye Mtukufu akesema: “Na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu.” Kwa hivyo, riziki ya kidunia humjia Muumini na Kafiri. Na ama riziki ya nyoyo kama vile elimu, imani, kumpenda Mwenyezi Mungu, kumnyenyekea, kumtumaini na mfano wa hayo, yeye hampi hayo isipokuwa yule ampendaye.