پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
سورهٔ ۲

Al-Baqara

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۱۸۰

كُتِبَ عَلَيْكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ ٱلْمَوْتُ إِن تَرَكَ خَيْرًا ٱلْوَصِيَّةُ لِلْوَٰلِدَيْنِ وَٱلْأَقْرَبِينَ بِٱلْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى ٱلْمُتَّقِينَ ۱۸۰

Yani Mwenyezi Mungu aliwafaradhishieni nyinyi, enyi kundi la Waumini, “mmoja wenu anapofikwa na mauti.” Yani sababu zake kama vile maradhi yanayokaribia kuangamiza, na kuwepo kwa sababu za maangamizo. Na alikuwa “ataacha heri” [yani mali] ambayo ni mali nyingi kwa mujibu wa desturi. Basi inamlazimu awausie wazazi wake wawili na jamaa wa karibu kwake kwa wema, kwa kadiri ya hali yake bila ya uharibifu. Na wala kumpa wa mbali zaidi peke yake na siyo wa karibu zaidi, bali awapange kulingana na ukaribu wao na haja zao. Na kwa sababu hii ndiyo alitumia ndani yake vitendo vya kuboresha. Na kauli yake, “ni haki juu ya wachamungu” inaonyesha ulazima wa hilo. Kwa sababu, haki ni kile kilichothubutu. Na Mwenyezi Mungu ameifanya kuwa ni miongoni mwa yale yenye kuleta uchamungu. Na jua ya kwamba wengi wa wafasiri wanaona kuwa Aya hii ilifutwa na Aya ya mirathi. Na baadhi yao wanaona kuwa inahusiana na wazazi wawili na jamaa ambao si warithi; ingawa hakuna dalili inayobainisha umahsusi huo. Katika suala hili, ni bora zaidi kusema: Hakika wasia hii ni kwa wazazi wawili na jamaa kwa ujumla, ila Mwenyezi Mungu Mtukufu alirudisha (maelezo yake yaamuliwe) kwa desturi ya sasa (ya watu). Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akawawekea viwango wazazi wawili wanaorithi na jamaa wengine wanaorithi wema huo katika Aya za mirathi. Baada ya kwamba (wema huo) ulikuwa kiujumla, na ikabaki hukumu kuhusu wale ambao hawakurithi miongoni mwa wazazi waliozuiliwa kurithi na wengineo ambao walizuiwa kwa sababu ya mtu au sifa fulani. Basi mtu ameamrishwa kuwafanyia wasia watu hawa, na wao ndio wanaostahiki zaidi wema wake. Na kauli hii umma umekubaliana juu yake, na kwayo kunapatikana kupatanisha kati ya zile kauli mbili zilizotangulia. Kwa sababu, kila mmoja ya wale wanaozisema kila mmoja wao aliona kitu, lakini mitazamo ikatofautiana. Na kwa huku kupatanisha, kunakuwa na kuafikiana na kupatanisha kati ya Aya hizi. Kwa sababu, kila inapowezekana kupatanisha inakuwa bora zaidi kuliko kudai kuwepo ufutaji ambao hauungwi mkono na dalili yoyote sahihi.