پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
سورهٔ ۲

Al-Baqara

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۱۵۱

كَمَآ أَرْسَلْنَا فِيكُمْ رَسُولًا مِّنكُمْ يَتْلُوا۟ عَلَيْكُمْ ءَايَـٰتِنَا وَيُزَكِّيكُمْ وَيُعَلِّمُكُمُ ٱلْكِتَـٰبَ وَٱلْحِكْمَةَ وَيُعَلِّمُكُم مَّا لَمْ تَكُونُوا۟ تَعْلَمُونَ ۱۵۱

(151) Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hakika neema yetu juu yenu kwa kuwaelekeza Al-Ka'aba na kuikamilisha kwa sheria na neema zinazokamilisha. Hilo siyo uvumbuzi mpya wa hisani yetu, wala la kwanza lake. Bali tumewaneemesha kwa misingi ya neema na yenye kuikamilisha, na ya juu yake zaidi ni kwamba, sisi tumekutumia huyu Mtume mtukufu kutoka miongoni mwenu. Mnaijua nasaba yake, ukweli wake, uaminifu wake, na ukamilifu wa nasaha yake, “anakusomeeni Aya zetu.” Na hili linajumuisha Aya za Qur-ani na mengineyo. Kwani, yeye anakusomeeni Aya zinazobainisha haki kutokana na batili, na uongofu kutokana na upotofu ambao zilikuonyesheni hapo mwanzo upweke wa Mwenyezi Mungu na ukamilifu wake. Kisha kwenye ukweli wa Mtume wake na ulazima wa kumuamini. Kisha kwenye yote aliyoyaeleza ya kufufuliwa na ghaibu, mpaka mkapata uwongofu kamili, na elimu ya yakini, “zetu na kuwatakasa.” Yani azitakase tabia zenu na nafsi zenu kwa kuzilea juu ya tabia nzuri, na kuzitakasa kutokana na maadili machafu. Na hilo ni kama kuwatakasa kutoka katika shirki hadi kwa Tauhid, na kutoka katika kujionyesha (riyaa) hadi katika ikhlas (kumwelekea Mwenyezi Mungu peke yake). Na pia kutoka kwa uongo hadi kwa ukweli, na kutoka katika khiyana hadi katika uaminifu. Na kutoka katika kiburi hadi katika unyenyekevu, na kutoka katika tabia mbaya hadi katika tabia njema, na kutoka katika chuki na kuhamana na kukatana hadi katika mapenzi, kuwasiliana, kupendana na yasiyokuwa hayo miongoni mwa aina utakaso. “Na kuwafundisha Kitabu,” yani Qur-ani, maneno yake na maana zake, “na hekima” ilisemwa kuwa ni Sunna. Na ikasemwa kuwa hekima ni kujua siri za Sheria na ufahamu wake, na kuteremsha mambo katika viwango vyake. Kwa hivyo kwa mujibu wa haya, inakuwa kufundishwa Sunna kumejumuishwa katika kufundishwa Kitabu. Kwa sababu Sunna inabainisha, inafasiri na inaieleza Qur-ani, “na kukufundisheni mliyokuwa hamyajui.” Kwa sababu kabla ya utume wake walikuwa katika upotofu ulio wazi, bila ya elimu wala vitendo. Basi kila elimu au kitendo walichopata umma huu kilikuwa kwa mikono yake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na kwa sababu yake ilikuwa hivyo. Kwa hivyo, neema hizi ndizo misingi ya neema zote. Nazo ndizo neema kubwa zaidi anazowapa waja wake. Basi kazi yao ni kumshukuru Mwenyezi Mungu juu yake, na kuzitekeleza. Ndio maana, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: