Al-Baqara
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَإِذِ ٱبْتَلَىٰٓ إِبْرَٰهِـۧمَ رَبُّهُۥ بِكَلِمَـٰتٍ فَأَتَمَّهُنَّ ۖ قَالَ إِنِّى جَاعِلُكَ لِلنَّاسِ إِمَامًا ۖ قَالَ وَمِن ذُرِّيَّتِى ۖ قَالَ لَا يَنَالُ عَهْدِى ٱلظَّـٰلِمِينَ ۱۲۴
(124) Mwenyezi Mungu anafahamisha kuhusu mja wake na rafiki mwendani wake Ibrahim, amani iwe juu yake, ambaye imekubaliwa juu ya Uimamu wake na utukufu wake; ambaye kila moja ya makundi ya Watu wa Kitabu wanadai, bali hata washirikina; kwamba Mwenyezi Mungu alimjaribu na akampa mtihani kwa maneno. Yani kwa maamrisho na makatazo, kama ilivyo ada ya Mwenyezi Mungu katika kuwajaribu waja wake, ili ibainike mwongo ambaye haimariki wakati wa majaribio na mtihani kutokana na mkweli ambaye cheo chake kinapanda, heshima yake inaongezeka na matendo yake yanatakasika; na ubongo wake wake unakuwa safi. Na aliyekuwa mtukufu wao zaidi katika nafasi hii ni Al-Khalil (rafiki mwendani wa Mwenyezi Mungu), amani iwe juu yake. Yeye alitimiza yale ambayo Mwenyezi Mungu alimjaribu kwayo, akayakamilisha na kuyatimiza, kwa hivyo akamshukuru kwa hilo. Na Mwenyezi Mungu hakuacha kumshukuru, na akasema: "Hakika Mimi nitakufanya uwe mwongozi wa watu." Yani watakufuata katika uwongofu, na watatembea nyuma yako kwenda kwa furaha yao ya milele, na unapata sifa ya kudumu; malipo makubwa na kutukuzwa na kila mtu. Na hii - ninaapa kwa umri wa Mwenyezi Mungu - ndiyo daraja bora zaidi ambayo washindani walishindania, na kituo cha juu kabisa ambacho wenye kutenda matendo walijiandaa kwa ajili yake. Na hali kamili zaidi iliyofikiwa na wale wenye stahamala kubwa miongoni mwa Mitume na wafuasi wao miongoni mwa kila mkweli anayewafuata; anayelingalia kwa Mwenyezi Mungu, na kwa njia yake. Ibrahim alipokifurahia cheo hiki, na akakipata , aliomba hilo kwa ajili ya kizazi chake, ili cheo chake na cheo cha kizazi chake kiinuke. Na hili pia ni kutokana na uongozi wake na nasaha zake kwa waja wa Mwenyezi Mungu na mapenzi yake kwamba waongofu wazidi kati yao. Basi utukufu ni kwa Mwenyezi Mungu kwa hima hizi za juu, na vyeo vya hali ya juu. Kwa hivyo, Mwenye huruma, Mpole akajibu na akafahamisha juu ya kizuizi cha kupata hiki cheo, akasema: "Ahadi yangu haitawafikia wenye kudhulumu." Yani uongozi katika dini hatapewa mwenye kuidhulumu nafsi yake, akaidhuru, na akaishushia hadhi, kwa sababu, dhuluma inapingana na cheo hiki. Kwa kuwa ni cheo ambacho chombo chake ni subira na yakini. Na matokeo yake ni kwamba mwenyewe awe upande mkubwa wa imani, matendo mema, tabia nzuri, maadili sahihi, upendo kamili, hofu, na toba. Basi iko wapi dhuluma na cheo hiki? Na ufahamu wa Aya uliashiria kwamba asiyedhulumu atapata uongozi, lakini kwa kufanya sababu zake.