Maryam
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
أَسْمِعْ بِهِمْ وَأَبْصِرْ يَوْمَ يَأْتُونَنَا ۖ لَـٰكِنِ ٱلظَّـٰلِمُونَ ٱلْيَوْمَ فِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ ۳۸
{38} "Watasikia na wataona vizuri vilivyoje Siku watakayotujia!" Kisha watakiri ukafiri wao na ushirikina wao na maneno yao, na watasema, "Mola wetu Mlezi! Tumeshaona, na tumeshasikia. Basi turejeshe tukatende mema, kwani hakika sisi tumekwisha kuwa na yakini sasa." Kwa hivyo, Siku ya Qiyama ndiyo watakuwa na yakini juu ya uhakika wa hali zao. "Lakini madhalimu sasa wamo katika upotovu ulio dhahiri" wala hawana udhuru wowote wa upotovu huu. Kwa sababu wako baina ya mtu mkaidi ambaye alipotea baada ya kufahamu vyema na akaijua haki lakini akaikataa, na kati ya yule aliyepotea njia ya haki, na tena anaweza kuijua haki na usahihi, lakini ameridhika na upotovu wake na matendo yake mabaya, hafanyi bidii ya kujua haki kutokana na batili. Na tazama jinsi alivyosema, "basi ole wao hao waliokufuru;" baada ya kauli yake, "Lakini makundi yakahitalifiana wao kwa wao." Wala hakusema, 'basi ole wao!' ili maneno hayo yayarudie makundi hayo yote. Kwa sababu miongoni mwa makundi hayo yaliyohitilafiana, kuna kundi [lililofuata usahihi] na likaafikiana na haki, na likasema kuhusiana na Isa kuwa yeye ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kwa hivyo wakamuamini na kumfuata. Basi hawa ni waumini na hawaingii katika ahadi hii ya adhabu. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akawaahidi makafiri tu ahadi hii ya adhabu.