Maryam
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
فَكُلِى وَٱشْرَبِى وَقَرِّى عَيْنًا ۖ فَإِمَّا تَرَيِنَّ مِنَ ٱلْبَشَرِ أَحَدًا فَقُولِىٓ إِنِّى نَذَرْتُ لِلرَّحْمَـٰنِ صَوْمًا فَلَنْ أُكَلِّمَ ٱلْيَوْمَ إِنسِيًّا ۲۶
{26} "Basi kula" tende, "na kunywa" kutoka mtoni, "na litulize jicho lako" kwa Issa. Na huu ndio utulivu wake katika suala la kuwa salama kutokana na uchungu wa kuzaa na kupata chakula na vinywaji vizuri. Na ama katika suala la maneno ya watu, akamuamrisha kwamba akimuona mtu yeyote, basi na aseme kwa ishara, "Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwingi wa rehema, ya kufunga." Yaani, kunyamaza, "kwa hivyo leo sitosema na mtu yeyote" haya ni ili asjipumzishe kutokana na maneno yao. Na siku hizo ilikuwa inajulikana kwao kwamba kunyamaza ni katika ibada za kisheria. Na hakuamrishwa kuwaongelesha katika suala hili na kujiondolea lawama, kwa sababu watu hawangemwamini, na tena hakuna faida yoyote katika kufanya hivyo, na ili kuwe kuondolewa kwake hatiani ni kupitia maneno ya Isa katika mlezi ni ushahidi mkubwa zaidi juu ya kutokuwa kwake na hatia. Na maana, mwanamke kuzaa mtoto bila mume na kudai kwamba hakutokana na mwanamume yeyote ni katika madai makubwa zaidi ambayo hata kama wataletwa mashahidi kadhaa, basi hangesadikiwa kwa hilo. Kwa hivyo ushahidi wa jambo hili lisilo la kawaida ukafanywa kutoka na jambo la aina yake, ambalo ni kuongea kwa Isa katika hali ya uchanga sana wake. Na ndiyo maana yeye Mtukufu akasema: