Al-Kahf
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
أَفَحَسِبَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ أَن يَتَّخِذُوا۟ عِبَادِى مِن دُونِىٓ أَوْلِيَآءَ ۚ إِنَّآ أَعْتَدْنَا جَهَنَّمَ لِلْكَـٰفِرِينَ نُزُلًا ۱۰۲
{102} Na huu ni uthibitisho na ubainisho wa ubatili wa madai ya washirikina makafiri, ambao waliwachukua baadhi ya manabii na vipenzi wa Mwenyezi Mungu kuwa washirika wa Mwenyezi Mungu wakawa wanawaabudu. Na wakadai kwamba watakuwa vipenzi walinzi wao, ili wawaokoe kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na wawape thawabu zake, nao walimkufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Basi Mwenyezi Mungu anawaambia kwa njia ya kuuliza na kukanusha kusikopingika kwa maana huo ni ubatili wake katika akili, "Je, wanadhani wale waliokufuru kwamba watawafanya waja wangu kuwa vipenzi wao?" Yaani, hilo haliwi, na wala kipenzi cha Mwenyezi Mungu kamwe hawezi kumfanya adui wa Mwenyezi Mungu. Kwa maana vipenzi wake wanakubaliana na Mwenyezi Mungu katika upendo wake, kuridhia kwake, hasira zake na chuki yake. Na kwa maana hii, aya hii inakuwa sawa na kauli yake yeye Mtukufu, "Na siku atakayowakusanya wote, kisha atawaambia Malaika: Je, hawa walikuwa wakiwaabudu nyinyi? Watasema: Subhanak (Umetakasika). Wewe ndiye kipenzi chetu, si hao." Kwa hivyo, yeyote yule anayedai kwamba amemchukua kipenzi cha Mwenyezi Mungu kuwa ni kipenzi wake ilhali yeye ni adui wa Mwenyezi Mungu, basi yeye ni mwongo. Na inawezekana kwamba - nayo hii ndiyo maana ya dhahiri - maana yake ni kuwa: Je, wale waliomkufuru Mwenyezi Mungu na kuwafanyia uadui Mitume wake kuwa watawafanya badala ya Mwenyezi Mungu, vipenzi wa kuwanusuru na kuwanufaisha kando na Mwenyezi Mungu na kuwazuia madhara? Hii ni dhana batili na mbovu. Kwa maana, viumbe vyote havina chochote mikononi mwao cha kunufaisha na kudhuru. Na hii ni kama kauli yake yeye Mtukufu, "Sema: Waombeni hao mnaowadaia badala yake Yeye. Hawawezi kuwaondolea madhara, wala kuyaweka pengine." "Wala hao ambao wao wanawaomba badala yake Yeye hawana uwezo wa kumwombea mtu." Na mfano wa hizo miongoni mwa Aya ambazo Mwenyezi Mungu anataja ndani yake kwamba yule anayechukuwa badala yake kipenzi ili amnusuru na kumlinda, ni mpotevu ambaye ameambulia patupu katika matarajio yake, ambaye hawezi pata baadhi ya makusudio yake. "Hakika Sisi tumeiandaa Jahannamu iwe ndipo pahali pa kuteremkia pa makafiri;" kama wageni na makaribisho kwao. Basi mashukio maovu mno ni mashukio yao hayo. Na makaribisho maovu mno ni hayo yao ya Jahannam.