Al-Israa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
قُلْ كُونُوا۟ حِجَارَةً أَوْ حَدِيدًا ۵۰ أَوْ خَلْقًا مِّمَّا يَكْبُرُ فِى صُدُورِكُمْ ۚ فَسَيَقُولُونَ مَن يُعِيدُنَا ۖ قُلِ ٱلَّذِى فَطَرَكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ ۚ فَسَيُنْغِضُونَ إِلَيْكَ رُءُوسَهُمْ وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هُوَ ۖ قُلْ عَسَىٰٓ أَن يَكُونَ قَرِيبًا ۵۱
{50 - 51} Na kwa sababu hiyo alimwamrisha Mtume wake -rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - kwamba awaambie hawa waliokanusha kufufuliwa kwa kuona kwamba hilo haliwezekani. "Sema: kuweni hata mawe na chuma. Au umbo lolote mnaloliona kubwa katika vifua vyenu." Ili msalimike kwa hilo - kwa madai yenu - kwamba nguvu za Mwenyezi Mungu hazitawafikia wala kwamba mapenzi yake hayatatekelezeka kwenu. Hakika nyinyi hamwezi kumshinda Mwenyezi Mungu katika hali yenu yoyote na katika sifa yoyote mnayoibadilikia. Nanyi wenyewe hamuwezi hata kuendesha chochote katika hali ya uhai wenu wala baada ya kifo. Basi acheni uendeshaji wa mambo na ubadilishaji wa mambo kwa Yule ambaye ni Muweza wa kila kitu na aliyezunguka kila kitu. "Watasema" wakati unapowasimamishia hoja juu ya ufufuo, "Ni nani atakayeturudisha tena? Sema: Yule yule aliyewaumba mara ya kwanza!" Kama alivyowaumba na hamkuwa chochote cha kukumbukwa, basi hakika yeye atawarudisha umbo jipya; "kama tulivyoanza umbo la kwanza, tutalirudisha tena." "Watakutikisia vichwa vyao" kwa kukataa na kushangazwa na kile ulichosema. "Watasema: Ni lini hayo?" Yaani, itakuwa lini saa ya kufufuliwa hiyo ambayo unadai kwa mujibu wa kauli yako? Si kwa kukiri asili ya ufufuo, bali huo ni upumbavu na kutaka kwao kushinda. "Sema: Labda itakuwa hivi karibuni" Na hakuna faida yoyote katika kubainisha wakati wake hasa, bali manufaa na mazingatio ni katika kuamini uhakika wa kutokea kwake na kulikubali hilo, na kulithibitisha, vinginevyo, kila kitu kinachokuja, basi hicho kiko karibu.