پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Israa
سورهٔ ۱۷

Al-Israa

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۲۸

وَإِمَّا تُعْرِضَنَّ عَنْهُمُ ٱبْتِغَآءَ رَحْمَةٍ مِّن رَّبِّكَ تَرْجُوهَا فَقُل لَّهُمْ قَوْلًا مَّيْسُورًا ۲۸

{28} Amri hii ya kuwapa jamaa ni kulingana na uwezo na utajiri. Ama ikiwa mtu hana na ana uchache katika kutekeleza matumizi ya sasa, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaamuru warudishe majibu mazuri. Akasema, "Na ikiwa utawapa mgongo, nawe unatafuta rehema ya Mola wako Mlezi unayoitaraji." Yaani, ikiwa utawapa mgongo usiwape kitu hadi wakati mwingine ambao unatarajia Mwenyezi Mungu kufanya mambo kuwa mepesi. "Basi sema nao maneno laini." Yaani, kwa upole na kutokuwa mgumu, na kuwapa ahadi ya kuwafanyia mazuri fursa itatokea na uombe udhuru wa kutoweza kufanya hivyo kwa wakati huu, ili waondoke kutoka kwako hali ya kuwa mawazo yao yametulia. Kama Mwenyezi Mtukufu alivyosema, "Kauli njema na usamehevu ni bora kuliko sadaka inayofuatiliwa na maudhi." Hili pia ni katika upole wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake, ambapo aliwaamuru wasubiri rehema na riziki kutoka kwake, kwa sababu kungojea hilo ni ibada. Na vile vile ahadi yao ya kutoa sadaka na kufanya wema katika hali ya wepesi ni ibada ya sasa. Kwa sababu kuazimia kufanya matendo mazuri ni jambo zuri. Na kwa hivyo mtu anapaswa kufanya kile anachoweza kufanya ya heri, na akusudie kufanya kile asichoweza kufanya ili alipwe kwa hilo, na labda Mwenyezi Mungu anaweza kumrahisishia kwa sababu ya tumaini lake.