پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nahl
سورهٔ ۱۶

An-Nahl

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیه‌های ۲۱–۲۲

أَمْوَٰتٌ غَيْرُ أَحْيَآءٍ ۖ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ ۲۱ إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَٰحِدٌ ۚ فَٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ قُلُوبُهُم مُّنكِرَةٌ وَهُم مُّسْتَكْبِرُونَ ۲۲

{21 - 22} Pamoja na hili, wao hawana chochote katika sifa za ukamilifu, wala elimu wala kinginecho. "Ni wafu, si wahai" Hawasikii, wala hawaoni, wala hawaelewi chochote. Basi je, hawa wanaweza kufanywa miungu badala ya Mola Mlezi wa walimwengu wote? Basi na ziangamie akili za washirikina! Ni upotofu mkubwa ulioje huu wao! Na mbovu mkubwa ulioje huu wao! Kwa maana, zilipotea kuhusiana na kitu kilicho dhahiri zaidi katika ubovu wake, na wakatoshanisha kati vilivyo vipungufu kwa namna zote visivyokuwa na sifa zozote za ukamilifu wala hawawezi kufanya chochote na yule ambaye ni mkamilifu kwa namna zote. Kwa maana ana elimu inayozunguka vitu vyote, na uwezo wa jumla, na rehema pana ambayo ilijaza walimwengu wote, na sifa njema, na utukufu, ukubwa, na ukuu ambao hakuna yeyote katika viumbe anayeweza kuzunguka baadhi ya sifa zake. Na ndiyo maana akasema, "Mungu wenu ni Mungu Mmoja" ambaye ni Mwenyezi Mungu, wa Pekee, Mmoja, Mkusudiwa, ambaye hakuzaa, wala hakuzaliwa, wala hana chcochote kinacholingana naye. Basi nyoyo za watu wa imani na akili zilimtukuza, na zikampa taadhima, na zikampenda kwa upendo mkubwa, na wakamfanyia kila kitu walichoweza miongoni mwa mambo ya kuwaweka karibu naye ya kimwili na kimali, na matendo ya mioyo, na matendo ya viungo, na wakamsifu kwa majina yake mazuri zaidi na sifa zake na matendo yake matakatifu. Na "wale wasioiamini Akhera nyoyo zao zinakataa" jambo hili kubwa, ambalo halikatai isipokuwa kiumbe ambaye ndiye mkubwa zaidi kwa ujinga na ukaidi. Na hili jambo ni upweke wa Mwenyezi Mungu. "Nao wanatakabari" kumfanyia ibada.