An-Nahl
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
فَإِذَا قَرَأْتَ ٱلْقُرْءَانَ فَٱسْتَعِذْ بِٱللَّهِ مِنَ ٱلشَّيْطَـٰنِ ٱلرَّجِيمِ ۹۸ إِنَّهُۥ لَيْسَ لَهُۥ سُلْطَـٰنٌ عَلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ ۹۹ إِنَّمَا سُلْطَـٰنُهُۥ عَلَى ٱلَّذِينَ يَتَوَلَّوْنَهُۥ وَٱلَّذِينَ هُم بِهِۦ مُشْرِكُونَ ۱۰۰
{98 - 100} Yaani, unapotaka kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu, ambacho ndicho kitabu cha heshima zaidi kitukufu zaidi, na ambacho ndani yake kuna yenye kufanya mioyo kutengenea, na elimu nyingi, basi shetani hutia bidii zaidi dhidi ya mja anapotaka kuanza kufanya mambo mema. Kwa hivyo anafanya bidii kubwa kumuondoa katika makusudi yake na maana zake. Kwa hivyo, njia ya usalama kutokana na uovu wake ni kumkimbilia Mwenyezi Mungu na kutafuta kinga yake kutokana na uovu wake. Kwa hivyo msomaji na aseme, "Ninajikinga kwa Mwenyezi Mungu kutoka na shetani aliyelaaniwa" huku akitafakari maana yake, akitemgemea Mwenyezi Mungu kwa moyo wake katika kumuondoa karibu naye, akijitahidi katika kuzuia wasiwasi wake na fikira zake mbaya, akifanya bidii kufanya sababu yenye nguvu zaidi ya kumzuia, ambayo ni kujipamba kwa pambo la imani na kumtegemea Mwenyezi Mungu. Kwa maana, Shetani "hana mamlaka juu ya wale walioamini na wakamtegemea Mola wao Mlezi" peke yake, asiyekuwa na mshirika yeyote. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu anawazuia waumini wanaomtegemea kutokana na uovu Shetani naye anabaki hana njia yoyote ya kuwafikia. "Hakika mamlaka yake yako juu ya wale wanaomfanya kuwa rafiki yao msaidizi" na hilo huwa kwa kuacha kumfanya Mwenyezi Mungu kuwa rafiki msaidizi, na kuingia katika utii wa Shetani, na kujiunga na kikundi chake. Basi wao wenyewe ndio waliomfanya kuwa rafiki yao msaidizi, naye akawachochea mchocheo mkubwa kuingia katika maasia, na akawaongoza kwelikweli kuingia motoni.