Ibrahim
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَبَؤُا۟ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ قَوْمِ نُوحٍ وَعَادٍ وَثَمُودَ ۛ وَٱلَّذِينَ مِنۢ بَعْدِهِمْ ۛ لَا يَعْلَمُهُمْ إِلَّا ٱللَّهُ ۚ جَآءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِٱلْبَيِّنَـٰتِ فَرَدُّوٓا۟ أَيْدِيَهُمْ فِىٓ أَفْوَٰهِهِمْ وَقَالُوٓا۟ إِنَّا كَفَرْنَا بِمَآ أُرْسِلْتُم بِهِۦ وَإِنَّا لَفِى شَكٍّ مِّمَّا تَدْعُونَنَآ إِلَيْهِ مُرِيبٍ ۹
{9} Yeye Mtukufu anasema akiwahofisha waja wake kwa yale aliyowatia umma waliokadhibisha walipojiwa na Mitume lakini wa wakawakadhibisha, basi akawaadhibu kwa adhabu ya haraka ambayo watu waliiona na kuisikia, kwa hivyo akasema: "Je, hazikuwajia habari za wale walio kabla yenu? Kaumu ya Nuhu, na 'Aadi, na Thamud" Na Mwenyezi Mungu alivitaja visa vyao katika Kitabu chake na akavipanua; "Na wale waliokuwa baada yao, ambao hakuna awajuaye isipokuwa Mwenyezi Mungu?" Kwa sababu ya wingi wao na habari zao zilipotelea mbali. Basi hao wote "Mitume wao waliwajia kwa hoja zilizo wazi" zenye kuonyesha ukweli wa yale waliyokuja nayo, kwani Mwenyezi Mungu hakumtuma Mtume yeyote isipokuwa alimpa ishara ambazo mfano wake wanadamu wanaziamini. Lakini hawa walipojiwa na Mitume wao na hoja zilizo wazi, hawakuzifuata, bali walizifanyia kiburi, "wakarudisha mikono yao kwenye vinywa vyao." Yaani, hawakuamini yale waliyowajia nayo, na wala hawakutamka lolote linaloashiria kuwa wameamini, kama kauli yake, "wakawa wanatia vidole vyao katika masikio yao kwa sababu ya mingurumo, kwa kuogopa kufa." "Na wakawaambia" waziwazi Mitume wao, "Hakika sisi tumeyakataa hayo mliyotumwa nayo, na hakika sisi tuna shaka kubwa na hayo mnayotuitia."