Yusuf
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
ثُمَّ يَأْتِى مِنۢ بَعْدِ ذَٰلِكَ عَامٌ فِيهِ يُغَاثُ ٱلنَّاسُ وَفِيهِ يَعْصِرُونَ ۴۹
{49} "Kisha utakuja baada ya hayo; yaani, ile miaka Saba Migumu "mwaka ambao watu watanyewa, na humo watakama vinywaji." Yaani, ndani yake kuna mvua na mafuriko yatakuwa nyingi, na mawimbi yataongezeka, na vyakula vyao vikuu vitazidi mazao kiasi kwamba watakama zabibu na mfano wake pamoja na chakula chao. Huenda dhana yake ya kuwepo mwaka huu wenye rutuba, ijapokuwa haijasemwa wazi wazi katika ndoto hiyo ya mfalme ni Kwa sababu inafahamika kutokana na [kukadiria] miaka saba ya dhiki kwamba mwaka unaofuata utaondoa shida zake. Na inavyojulikana ni kwamba ukame wenye kuendelea kwa miaka saba mfululizo hautoweki isipokuwa kwa mwaka wenye rutuba sana. Vinginevyo, kwa kukadiria huku hakungekuwa na manufaa. Na yule mjumbe aliporudi kwa mfalme na watu, na akawajulisha kuhusu tafsiri ya Yusufu ya ndoto hiyo, walistaajabishwa na hilo, na wakafurahi kufurahi kukubwa sana.