Yusuf
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَٱتَّبَعْتُ مِلَّةَ ءَابَآءِىٓ إِبْرَٰهِيمَ وَإِسْحَـٰقَ وَيَعْقُوبَ ۚ مَا كَانَ لَنَآ أَن نُّشْرِكَ بِٱللَّهِ مِن شَىْءٍ ۚ ذَٰلِكَ مِن فَضْلِ ٱللَّهِ عَلَيْنَا وَعَلَى ٱلنَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ ۳۸
{38} "Na nimefuata mila ya baba zangu, Ibrahim, na Is-haq, na Yaa'qub" kisha akaieleza mila hiyo kwa kauli yake "Haikutufailia sisi." [Yaani, haikuwa inaendana nasi] "kumshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote." Bali sisi tunampwekesha Mwenyezi Mungu kwa tauhidi na tunamfanyia yeye tu dini yetu na ibada. "Hiyo ni katika fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yetu na juu ya watu." Yaani, hii ni katika bora zaidi miongoni mwa [neema] yake na ihsani yake juu yetu na juu ya wale ambao Mwenyezi Mungu amewaongoa kama alivyotuongoa. Kwani, hakuna bora zaidi kuliko neema ya Mwenyezi Mungu juu ya waja wake kwa Uislamu na Dini iliyonyooka. Kwa hivyo, mwenye kuikubali na kuifuata, basi hiyo ni bahati yake, na atakuwa amepata neema kubwa zaidi na na fadhila tukufu zaidi; "Lakini wengi wa watu hawashukuru." Na ndiyo maana neema na ihsani zinawajia, lakini hawazikubali na hawamtimizii Mwenyezi Mungu haki yake. Na katika hili kuna kutia moyo juu ya kushika njia ambayo yeye yuko juu yake kwa mbinu ambayo haifichiki. Kwa maana, wale vijana wawili alipokwisha jua kwamba walimuona kwa jicho la taadhima na heshima kubwa na kwamba alikuwa mwema na mwalimu, akawatajia kuwa hali hii niliyo nayo ni kwa sababu ya fadhila na ihsani ya Mwenyezi Mungu; kwa kuwa alinineemesha kwa kuacha ushirikina na kufuata mila ya baba zangu. Na kwa sababu ya haya ndio nikafikia kile mlichokiona, kwa hivyo mnapaswa kufuata kile nilichokifanya.