Yusuf
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
قُلْ هَـٰذِهِۦ سَبِيلِىٓ أَدْعُوٓا۟ إِلَى ٱللَّهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا۠ وَمَنِ ٱتَّبَعَنِى ۖ وَسُبْحَـٰنَ ٱللَّهِ وَمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلْمُشْرِكِينَ ۱۰۸
{108} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad -rehema na amani ya Mwenyezi Mungu zimshukie: - "Sema," uwaambie watu: "Hii ndiyo njia yangu;" yaani, njia yangu ninayoilingania, nayo ni njia inayofikisha kwa Mwenyezi Mungu na kwenye nyumba ya utukufu wake, ambayo inajumuisha kuijua haki na kuifanyia kazi na kuipendelea, na kumfanyia dini Mwenyezi Mungu peke yake bila mshirika yeyote. "Ninalingania kwa Mwenyezi Mungu;” yaani, ninawahimiza viumbe na waja wamfikie Mola wao Mlezi, na ninawatia moyo juu ya hilo, na ninawahofisha dhidi ya yale yatakayowaweka mbali naye, na pamoja na hayo, mimi ninafanya hayo “kwa ufahamu mzuri” na yakini kuhusu dini yangu bila shaka yoyote. Na vile vile “wale wanaonifuata” wanalingania kwa Mwenyezi Mungu kama vile ninavyolingania kwa ufahamu mzuri wa mambo yake. "Na Mwenyezi Mungu ametakasika” kutokana na yale aliyonasibishwa nayo miongoni mwa yale yasiyoufailia utukufu wake au kupingana na ukamilifu wake. "Wala mimi si katika washirikina” katika mambo yangu yote, bali mimi ninamwabudu Mwenyezi Mungu kwa kumkusudia Yeye tu katika Dini yangu.