Hud
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
قَالُوا۟ يَـٰصَـٰلِحُ قَدْ كُنتَ فِينَا مَرْجُوًّا قَبْلَ هَـٰذَآ ۖ أَتَنْهَىٰنَآ أَن نَّعْبُدَ مَا يَعْبُدُ ءَابَآؤُنَا وَإِنَّنَا لَفِى شَكٍّ مِّمَّا تَدْعُونَآ إِلَيْهِ مُرِيبٍ ۶۲
{62} Basi Nabii wao Saleh amani iwe juu yake alipowaamrisha na akawahimiza wamkusudie Mwenyezi Mungu peke yake, wakaukataa wito wake huo, na wakaukabili kuukabili kubaya zaidi. Na "Wakasema: Ewe Saleh! Hakika kabla ya haya ulikuwa unatarajiwa heri kwetu." Yaani, tulikuwa tukikutarajia na kuwa na matumaini nawe kwamba una akili na manufaa. Na huu ni ushahidi kutoka kwao kwa Nabii wao Saleh kwamba hakuacha kujulikana kwa tabia njema na maadili ya hali ya juu, na kwamba yeye ni miongoni mwa walio bora zaidi wa kaumu yake, lakini alipowajia na jambo hili ambalo halikukubaliana na matamanio yao maovu. Wakasema maneno haya ambayo makusudio yake ni kwamba wewe hakika ulikuwa mkamilifu, na sasa umeyafelisha maoni yetu kuhusiana nawe, na umekuwa katika hali ambayo hakuna heri yoyote inayotarajiwa kutoka kwako. Na dhambi yake ni yale waliyosema juu yake, [ambayo ni kauli yao]: "Je unatukataza kuwaabudu wale ambao baba zetu walikuwa wakiwaabudu?" Na kulingana na madai yao ni kwamba hilo ni miongoni mwa doa kubwa zaidi kwa Saleh. Vipi alikashifu akili zao na akili za baba zao wapotovu? Na vipi anawakataza kuwaabudu wale ambao hawanufaishii, wala hawadhuru, wala hawasaidii kitu, miongoni mwa mawe, na miti, na mfano wake, na akawaamrisha kumfanyia dini Mwenyezi Mungu tu, Mola wao Mlezi ambaye neema zake juu yao hazijaacha kufuatana, na kuteremka kwa wema wake juu yao kwa daima, na ambaye hakuna neema yoyote isipokuwa ni kutoka kwake, wala hakuna yeyote anayewazuia kutokana na mabaya isipokuwa Yeye? "Na hakika sisi tuna shaka na wasiwasi kwa hayo unayotuitia." Yaani, bado tuko katika shaka juu ya yale uliyotulingania. Nayo ni shaka inayotia kusitasita kukubwa mioyoni mwetu.