Hud
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
إِلَّا مَن رَّحِمَ رَبُّكَ ۚ وَلِذَٰلِكَ خَلَقَهُمْ ۗ وَتَمَّتْ كَلِمَةُ رَبِّكَ لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ ٱلْجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ أَجْمَعِينَ ۱۱۹
{119} "Isipokuwa wale ambao Mola wako Mlezi amewarehemu." Basi akawaongoa kwenye elimu ya Haki, na kuifanyia kazi, na kuafikiana juu yake. Basi hawa yalikwisha watangulia matangulizi ya furaha na wakafikiwa na uangalizi wa kiungu, na kuwezeshwa wa kiungu. Na ama wale wasiokuwa wao, hao waliachiliwa mbali wajisimamie wenyewe. Na kauli yake: "Na kwa hiyo ndiyo Mwenyezi Mungu amewaumba." Yaani, ilihitaji Hekima yake kuwa aliwaumba ili miongoni mwao kuwe na wenye furaha na walioko mashakani, na wenye kuafikiana na wenye kuhitalifiana, kundi aliloliongoa Mwenyezi Mungu, na kundi ambalo upotevu uliwathibitikia, ili iwabainikie waja uadilifu wake na hekima Yake, na ili ayadhihirishe mazuri na maovu yaliyokuwa yamejificha katika maumbile ya wanadamu, na lisimame suala la jihadi na ibada zisizoweza kukamilika wala kunyooka isipokuwa kwa njia ya mitihani na majaribio "na" kwa sababu "lilitimia neno la Mola wako Mlezi kwamba hakika nitaijaza Jahannam kwa majini na watu kwa pamoja." Basi ni lazima ausahilishie Moto huo wastahiki wake wanaofanya matendo yake yafikishayo humo.