پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Yunus
سورهٔ ۱۰

Yunus

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۴

إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا ۖ وَعْدَ ٱللَّهِ حَقًّا ۚ إِنَّهُۥ يَبْدَؤُا۟ ٱلْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥ لِيَجْزِىَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ بِٱلْقِسْطِ ۚ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَهُمْ شَرَابٌ مِّنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌۢ بِمَا كَانُوا۟ يَكْفُرُونَ ۴

{4} Alipotaja hukumu yake ya kimajaliwa, ambayo ni uendeshaji wa jumla, na hukumu yake ya kidini, ambayo ni sheria yake, ambayo madhumuni yake na makusudio yake ni kumwabudu yeye peke yake, bila mshirika yeyote, akataja hukumu ya kimalipo, ambayo ni malipo yake kwa matendo baada ya kufa. Akasema: "Kwake Yeye tu ndiyo marejeo yenu nyote.” Yaani, atawakusanya baada ya kufa kwenu kwa ajili ya wakati na siku maalumu. "Hakika Yeye ndiye anayeanzisha uumbaji, kisha ataurejesha” kwa maana Mwenye uwezo wa kuanzisha uumbaji ni muweza wa kuurudisha. Na mwenye kuona kuanza kwake uumbaji kisha akakanusha kurudisha kwake uumbaji, basi hana akili, ni mwenye kukanusha mojawapo ya mawili yanayofanana, pamoja na kuthibitisha kwake kile kinachofaa zaidi ya hilo analolikanusha. Basi huu ni ushahidi ulio wazi wa kiakili juu ya kurudishwa kwa uumbaji (Siku ya Qiyama). Kisha akataja ushahidi wa kimaandiko, akasema: "Hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyo ya kweli;” yaani, ni Ahadi yake ya ukweli, na ni lazima itimizwe, “ili awalipe kwa uadilifu wale walioamini” kwa nyoyo zao yale aliyowaamrisha Mwenyezi Mungu kuyaamini, “na wakatenda mema” kwa viungo vyao miongoni mwa wajibu mbalimbai na yale yanayopekezwa. “Kwa uadilifu,” yaani: kwa imani yao na vitendo vyao, malipo ambayo alikwisha wabainishia waja wake na akajulisha kuwa hakuna nafsi yoyote inayojua waliyofichiwa miongoni mwa yale yafurahishayo macho. "Na wale waliokufuru” Aya za Mwenyezi Mungu, na wanawakadhibisha Mitume wa Mwenyezi Mungu, “wana vinywaji vya maji ya moto” yenye kubambua nyuso na kukata matumbo, "na adhabu chungu” kutoka kwa kila aina ya adhabu zinginezo “kwa sababu ya yale waliyokuwa wakikufuru.” Yaani, kwa sababu ya ukafiri wao na dhuluma yao. Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, bali wanajidhulumu wenyewe.