القلم
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَإِن يَكَادُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَيُزْلِقُونَكَ بِأَبْصَـٰرِهِمْ لَمَّا سَمِعُوا۟ ٱلذِّكْرَ وَيَقُولُونَ إِنَّهُۥ لَمَجْنُونٌ ٥١ وَمَا هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَـٰلَمِينَ ٥٢
{51 - 52} Basi Mtume wetu Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie - akatekeleza amri ya Mwenyezi Mungu, na akavumilia hukumu ya Mola wake Mlezi kwa subira asiyoweza kuifahamu yeyote katika walimwengu. Basi Mwenyezi Mungu akamfanyia mwisho mwema, na hakika mwisho ni kwa wacha Mungu, na maadui zake hawakupata chochote katika hilo ila yale yaliyowawiya mabaya sana, kiasi kwamba wakawa na hamu kubwa ya kumtelezesha "kwa macho yao" kutokana na husuda, chuki na hasira zao. Hiki ndicho kiwango cha mwisho cha madhara halisi waliyoweza kuyafanya, na Mwenyezi Mungu ndiye mlinzi na msaidizi wake. Ama madhara ya kimaneno, wao walisema mambo juu yake kulingana na yale ambayo nyoyo zao ziliwataka kusema. Basi mara wakasema: 'Yeye ni kichaa!' mara 'Mshairi!' mara: 'Mchawi!' Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote." Yaani, Qur-ani hii tukufu na Ukumbusho wenye hekima si chochote ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote, ambao kwayo wanakumbuka masilahi ya dini yao na dunia yao, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.