انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · القلم
السورة ٦٨

القلم

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ١–٢

نٓ ۚ وَٱلْقَلَمِ وَمَا يَسْطُرُونَ ١ مَآ أَنتَ بِنِعْمَةِ رَبِّكَ بِمَجْنُونٍ ٢

{1 - 2} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaapa kwa kalamu, nalo ni jina la jenasi linalojumuisha kalamu ambazo aina mbalimbali za elimu zinaandikwa kwazo, na ambazo kwazo nathari na mashairi yanaandikwa. Hilo ni kwa sababu kalamu na vyote vinavyotumika katika kuandika aina mbalimbali za maneno ni miongoni mwa ishara zake kubwa, ambazo kwazo [Mwenyezi Mungu] anastahiki kuapa kwazo juu kwa kuwa mbali kwa Nabii wake – Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani – kutokana na wendawazimu waliomnasibisha nao maadui zake. Basi akamkanushia kwa neema ya Mola wake Mlezi juu yake na wema wake. Ambapo alimneemesha akili kamilifu, maoni ya sawasawa na usemi wenye maamuzi ya kukata, ambao ndicho bora zaidi ambacho kalamu ziliwahi kuandika na kuandikwa na wanadamu, na hili ndilo furaha katika dunia.