انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٦٣

قُلْ مَن يُنَجِّيكُم مِّن ظُلُمَـٰتِ ٱلْبَرِّ وَٱلْبَحْرِ تَدْعُونَهُۥ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً لَّئِنْ أَنجَىٰنَا مِنْ هَـٰذِهِۦ لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلشَّـٰكِرِينَ ٦٣

{63} Yaani: "Sema," uwaambie wale wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu, wanaoomba pamoja naye miungu mingine, ukiwalazimisha kwa yale waliyoyathibitisha ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika Umola wake kwa yale waliyoyakanusha ya kumpwekesha katika Uungu. "Ni nani huwaokoa kutoka katika giza mbalimbali la nchi kavu na baharini?" Yaani, shida zake na ugumu wake, na wakati inaposhindikana au inakuwa vigumu njia ya kufanya hila. Basi mkawa mnamwomba Mola wenu Mlezi kwa moyo ulionyenyekea na ulimi ambao hauachi kusema haja yake katika dua, na mnasema huku mkiwa katika hali hiyo: "Akituokoa tu kutoka katika hili," la ugumu ambao tuko ndani yake, "bila shaka tutakuwa miongoni mwa wenye shukrani" kwa Mwenyezi Mungu. Yaani, wale wanaoikubali neema yake, na wanaoiweka kumtii Mola wao Mlezi, wale walioihifadhi ili wasiitumie katika kumuasi.