انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٦

أَلَمْ يَرَوْا۟ كَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَبْلِهِم مِّن قَرْنٍ مَّكَّنَّـٰهُمْ فِى ٱلْأَرْضِ مَا لَمْ نُمَكِّن لَّكُمْ وَأَرْسَلْنَا ٱلسَّمَآءَ عَلَيْهِم مِّدْرَارًا وَجَعَلْنَا ٱلْأَنْهَـٰرَ تَجْرِى مِن تَحْتِهِمْ فَأَهْلَكْنَـٰهُم بِذُنُوبِهِمْ وَأَنشَأْنَا مِنۢ بَعْدِهِمْ قَرْنًا ءَاخَرِينَ ٦

{6} Kisha akawaamrisha wazingatie kwa umma waliotangulia, kwa hivyo akasema, "Je, hawakuona ni vizazi vingapi tulivyoviangamiza kabla yao?" Yaani, ni mara ngapi kumefuatana kuangamiza kwetu umma zinazokadhibisha na tukawapa muhula kabla ya maangamizo hayo, kwamba, "Tuliwaimarisha katika dunia namna ambavyo hatukuwaimarisha" hawa kwa mali, na watoto, na starehe. “Na tukawatumia mvua nyingi na tukaifanya mito inapita kwa chini yao.” Ikawa inawaoteshea mazao na matunda alivyotaka Mwenyezi Mungu wakawa wanastareheka kwayo na walikula kwayo wanavyotamani, lakini hawakumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema zake. Bali waliyageukia matamanio na wakapumbazwa na [aina mbalimbali za] ladha, kisha wakawajia Mitume wao na hoja zilizo wazi, lakini hawakuzisadiki, bali walizikataa na wakazikadhibisha. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa dhambi zao, na akaanzisha kizazi kingine baada yao. Basi huu ndio mwenendo wa Mwenyezi Mungu na ada yake katika umma zilizotangulia na zilizofuata. Basi zingatieni kutoka kwa wale ambao Mwenyezi Mungu aliwasimulia habari zao.