انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٥

فَقَدْ كَذَّبُوا۟ بِٱلْحَقِّ لَمَّا جَآءَهُمْ ۖ فَسَوْفَ يَأْتِيهِمْ أَنۢبَـٰٓؤُا۟ مَا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ ٥

{5} "Basi hakika walikwisha ikadhibisha haki ilipowajia." Na haki ni haki yake kwamba, ifuatwe na ashukuriwe Mwenyezi Mungu kwa kuwafanyia wepesi na kuileta kwao. Lakini wao wakaikabili kwa kinyume cha anavyopasa kuikabili, kwa hivyo wakastahiki adhabu kali. "Kwa hivyo, zitawajia habari za yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha." Yaani, wataona yale waliyoyafanyia mzaha kwamba ndiyo haki na ukweli, na Mwenyezi Mungu atawabainishia waliokadhibisha kukadhibisha kwao, na kuzua kwao, na walikuwa wakiufanyia mzaha Ufufuo, na Pepo, na Moto. Basi itakapokuwa ni Siku ya Kiyama, wale waliokadhibisha Wataambiwa. Huu ndio Moto ambao mlikuwa mkiukadhibisha. Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na waliapa kwa Mwenyezi Mungu ukomo wa viapo vyao kwamba Mwenyezi Mungu hatomfufua aliyekufa. Sivyo hivyo! Ni ahadi ya haki iliyo juu yake; lakini wengi wa watu hawajui. Ili awabainishie yale wanayohitalifiana ndani yake, na ili wajue wale waliokufuru kwamba wao hakika walikuwa ni waongo}.