انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٥٤

وَإِذَا جَآءَكَ ٱلَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِـَٔايَـٰتِنَا فَقُلْ سَلَـٰمٌ عَلَيْكُمْ ۖ كَتَبَ رَبُّكُمْ عَلَىٰ نَفْسِهِ ٱلرَّحْمَةَ ۖ أَنَّهُۥ مَنْ عَمِلَ مِنكُمْ سُوٓءًۢا بِجَهَـٰلَةٍ ثُمَّ تَابَ مِنۢ بَعْدِهِۦ وَأَصْلَحَ فَأَنَّهُۥ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ٥٤

{54} Na Mwenyezi Mungu alipomkataza Mtume wake kuwafukuza Waumini watiifu, Akamuamrisha kuamiliana nao kwa ukarimu, na taadhima, na utukufu, na heshima. Kwa hivyo akasema: "Na wanapokujia wanaoziamini Ishara zetu waambie: Assalamu alaikum! (Amani iwe juu yenu!)" Yaani, na Waumini wanapokujia, basi wasalimie, na wapokee, na wape maakizi kutoka kwako na amani, na wape bishara ya yale yatakayoamsha azima yao na hima zao miongoni mwa rehema ya Mwenyezi Mungu na ukarimu wake mwingi na ihsani yake. Na wahimize juu ya kufuata kila sababu na njia inayofikisha katika hayo, na wahofishe dhidi ya kudumu katika madhambi. Na waamrishe watubie madhambi ili wapate kufutiwa dhambi na Mola wao Mlezi na ukarimu wake mwingi. Na ndiyo maana akasema, "Mola wenu Mlezi amejilazimisha rehema, ya kwamba atakayefanya uovu miongoni mwenu kwa ujinga, kisha akatubu baada yake na akatengenea. Yaani, hapana budi pamoja na kuacha madhambi, na kujiepusha nayo na kuyajutia, kurekebisha matendo na kutekeleza yale ambayo mwenyezi Mungu aliyowajibisha, na kurekebisha yale ambayo yaliharibika katika matendo ya dhahiri na yale yaliyofichika. Na ikiwa yote haya yatapatikana, basi "hakika Yeye ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu"; Yaani, Atawamiminia katika kufuta dhambi kwake, na rehema yake kulingana na yale waliyoyatenda miongoni mwa yale aliyowaamrisha.