الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَقَالُوا۟ لَوْلَا نُزِّلَ عَلَيْهِ ءَايَةٌ مِّن رَّبِّهِۦ ۚ قُلْ إِنَّ ٱللَّهَ قَادِرٌ عَلَىٰٓ أَن يُنَزِّلَ ءَايَةً وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ٣٧
{37} "Na walisema;" yaani, wale waliomkadhibisha Mtume kwa usugu na ukaidi, "kwa nini hakuteremshiwa muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi?" Wakimaanisha kwa hilo Aya za mapendekezo wanazozipendekeza wao kwa akili zao mbovu na maoni potovu. Kama kauli yao, "Na walisema; Hatutakuamini mpaka ututimbulie chemchem katika ardhi hii. Au uwe na bustani ya mitende na mizabibu, na utupasulie mito kati yake ikimiminika. Au utuangushie mbingu vipande vipande kama ulivyodai; au utuletee Mwenyezi Mungu na Malaika uso kwa uso..." hadi mwisho wa Aya. "Sema" ukiwajibu kauli yao: "Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuteremsha muujiza." Kwani hakuna upungufu wa kufanya hivyo katika uwezo Wake, vipi na ilhali vitu vyote vinafuata kwa sababu ya nguvu zake, na vinanyenyekea kwa sababu ya mamlaka yake. Lakini wengi wa watu hawajui, na hivyo wao kwa sababu ya ujinga wao na kutojua kwao, wanataka kile ambacho ni shari kwao miongoni mwa ishara ambazo lau zitawajia na wasiziamini, basi wangeharakishiwa adhabu. "Na hapana mnyama yeyote katika ardhi, wala ndege anayepaa kwa mbawa zake mbili, isipokuwa ni umma kama nyinyi. Hatukupuuza chochote katika Kitabu. Kisha kwa Mola wao Mlezi watakusanywa." Na kwa adhabu kama ilivyo ni Sunna ya mwenyezi Mungu ambayo haiwezi kubadilishwa. Na pamoja na hili, ikiwa makusudio yao ni Aya zinazowabainishia Haki na zinazowawekea njia wazi, basi hakika Muhammad - Swalah na salamu zimshukie - alikwisha kuja na kila Aya ya mkato, na hoja iliyo wazi inayoonyesha yale aliyokuja nayo ya haki; kiasi kwamba mja anaweza katika kila suala la dini kupata katika yale aliyoleta ushahidi kadhaa wa kiakili na wa kimaandiko, kiasi kwamba haibaki katika mioyo shaka hata kidogo na kusitasita. Basi ni mwingi wa baraka yule aliyemtuma Mtume wake na uwongofu na dini ya haki, na akaiunga mkono kwa Aya zilizo wazi. Ili mwenye kuangamia aangamie kwa hoja iliyo wazi, na mwenye kubaki hai abaki hai kwa hoja iliyo wazi, na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye elimu ya yote.