الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَإِن كَانَ كَبُرَ عَلَيْكَ إِعْرَاضُهُمْ فَإِنِ ٱسْتَطَعْتَ أَن تَبْتَغِىَ نَفَقًا فِى ٱلْأَرْضِ أَوْ سُلَّمًا فِى ٱلسَّمَآءِ فَتَأْتِيَهُم بِـَٔايَةٍ ۚ وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَمَعَهُمْ عَلَى ٱلْهُدَىٰ ۚ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلْجَـٰهِلِينَ ٣٥
{35} "Na ikiwa ni makubwa kwako huku kupeana kwao mgongo." Yaani, ikiwa ni vigumu kwako kwa sababu ya hima yako kubwa juu yao, na upendo wako kuona wakiamini, basi jitahidi katika hilo. Lakini si katika uwezo wako kumwongoa yule ambaye Mwenyezi Mungu hakutaka kumwongoa. "Basi kama unaweza kutafuta njia ya chini kwa chini ya ardhi, au ngazi kwendea mbinguni ili uwaletee Ishara." Yaani, fanya hivyo; kwani haitawanufaisha chochote. Na katika hili kuna kukata matumaini yake katika kuongoa mfano wa hawa wakaidi. "Na lau Mwenyezi Mungu angelitaka, angeliwakusanya juu ya uwongofu." Lakini hekima yake Yeye Mtukufu ilitaka kwamba wabaki katika upotofu. "Basi kamwe usiwe miongoni mwa wajinga;" wale wasiojua uhakika wa mambo na wala hawayaingizi katika nafasi zake.