انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الحديد
السورة ٥٧

الحديد

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٧

ءَامِنُوا۟ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَأَنفِقُوا۟ مِمَّا جَعَلَكُم مُّسْتَخْلَفِينَ فِيهِ ۖ فَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مِنكُمْ وَأَنفَقُوا۟ لَهُمْ أَجْرٌ كَبِيرٌ ٧

{7} Mwenyezi Mungu anawaamrisha waja wake kumwamini Yeye na Mtume wake na aliyoyaleta, na watoe mali kwa ajili ya njia Yake kutokana na mali ambazo Mwenyezi Mungu ameweka mikononi mwao na akawafanya kuwa wasimamizi juu wake. Ili aone jinsi wanavyofanya matendo. Kisha alipowaamuru kufanya hivyo, akawatia moyo na akawahimiza kufanya hivyo kwa kutaja malipo aliyowapangia, juu yake, akasema: "Basi wale walioamini miongoni mwenu, na wakatoa, wana malipo makubwa." Yaani, wale waliojumuisha kati ya kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kutoa mali kwa ajili ya njia yake kwamba watapata malipo makubwa, matukufu ambayo ni kuridhiwa na Mola wao Mlezi na kupata nyumba ya utukufu wake na neema ya milele aliyowaandalia Mwenyezi Mungu Waumini na Mujahidina (wanaopambana kwa ajili yake).