الحديد
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يُولِجُ ٱلَّيْلَ فِى ٱلنَّهَارِ وَيُولِجُ ٱلنَّهَارَ فِى ٱلَّيْلِ ۚ وَهُوَ عَلِيمٌۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ ٦
{6} "Anaingiza usiku katika mchana, na anaingiza mchana katika usiku." Yaani, usiku unaingia katika mchana, kisha unawafunika kwa giza lake, kwa hivyo wanatulia tuli. Kisha mchana unaingilia usiku, na giza lililoko kwenye ardhi linatoweka, na ulimwengu unaangazwa kwa hivyo waja wanatembea huku na kule, wakienda katika masilahi yao na mambo ya maisha yao. Na Mwenyezi Mungu anaendelea kuufunika usiku juu ya mchana, na kuufunika mchana juu ya usiku, na anavizungusha kwa kuongezeka na kupungua, kwa urefu na ufupi, mpaka misimu ipatikane kwa hayo na nyakati zinyooke sawa, ndiyo yapatikane masilahi mbalimbali kwa hayo. Basi ametakasika Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote. Na ametukuka Mwenye ukarimu, Mwenye kutoa kwa wingi, ambaye amewaneemesha waja wake kwa neema za dhahiri na zilizofichika. "Na Yeye ni Mwenye kuyajua mno yaliyomo vifuani" mwa walimwengu. Kwa hivyo, anamuwezesha anayejua kwamba anafailia hilo, na anamfelisha anayejua kwamba hafailii kuongolewa.