انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المائدة
السورة ٥

المائدة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٧٣

لَّقَدْ كَفَرَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓا۟ إِنَّ ٱللَّهَ ثَالِثُ ثَلَـٰثَةٍ ۘ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّآ إِلَـٰهٌ وَٰحِدٌ ۚ وَإِن لَّمْ يَنتَهُوا۟ عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ٧٣

{73} "Hakika, wamekufuru wale waliosema," Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa watatu." Na haya ni miongoni mwa maneno ya Wakristo walioshinda wanayoyatetea sana. Walidai kuwa Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa watatu: Mwenyezi Mungu, na Isa na Maryam! Ametukuka Mwenyezi Mungu juu ya maneno yao, kutukuka kukubwa. Na huu ndio ushahidi mkubwa zaidi juu ya uchache akili wa Wakristo. Je, walikubali vipi maneno haya mbaya, na itikadi mbaya? Vipi Muumba aliwafanania na kiumbe? Vipi Mola Mlezi wa walimwengu wote alifichikana kwao? Yeye Mtukufu alisema akiwapinga, na wale walio mfano wao: "Hali hakuna mungu isipokuwa Mungu Mmoja tu," anayesifika kwa kila sifa kamilifu, aliyetakasika na kila upungufu, mpweke katika uumbaji na kuendesha mambo." Na hakuna neema yoyote waliyo nayo viumbe isiokuwa ni kutoka kwake. Basi vipi atafanywa mungu mwingine pamoja naye? Mwenyezi Mungu ametukuka juu ya wanayosema madhalimu kutukuka kukubwa. Kisha akawaahidi adhahu kwa kauli yake; “Na ikiwa hawayaachi hayo wanayoyasema, basi kwa yakini itawagusa wale waliokufuru miongoni mwao adhabu chungu."