المائدة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لَقَدْ كَفَرَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓا۟ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْمَسِيحُ ٱبْنُ مَرْيَمَ ۖ وَقَالَ ٱلْمَسِيحُ يَـٰبَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ رَبِّى وَرَبَّكُمْ ۖ إِنَّهُۥ مَن يُشْرِكْ بِٱللَّهِ فَقَدْ حَرَّمَ ٱللَّهُ عَلَيْهِ ٱلْجَنَّةَ وَمَأْوَىٰهُ ٱلنَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّـٰلِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ ٧٢
{72} Yeye Mtukufu anajulisha juu ya ukafiri wa Wakristo kwa kauli yao, "hakika, Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu!" Kwa dhana potofu kuwa ametokana na mama bila ya baba, na akahalifu kuumba kwa kawaida kwa Mwenyezi Mungu. Na hali ya kweli ni kwamba yeye, rehema na amani ziwe juu yake, aliwakadhibisha katika madai hayo na akawaambia. "Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi." Kwa hivyo akajithibitishia yeye mwenyewe uja kamili, na umoja unaojumuisha viumbe wote kwa Mola wake Mlezi. "Hakika, mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu," na chochote miongoni mwa viumbe, si Isa wala mwengineye; "basi hakika, Mwenyezi Mungu amekwisha mharimishia Pepo, na pahali pake ni Motoni." Na hilo ni kwa sababu aliwasawazisha viumbe na Muumba, na akapeleka kile alichoumbwa kwa ajili yake, nacho ni kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake kwa yule ambaye si yake, kwa hivyo akastahiki kudumu katika Moto. "Na waliodhulumu hawatakuwa na wowote wa kuwanusuru." wataowaokoa kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu, au kuwazuia baadhi ya yale yaliyowasibu.