انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المائدة
السورة ٥

المائدة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَوْفُوا۟ بِٱلْعُقُودِ ۚ أُحِلَّتْ لَكُم بَهِيمَةُ ٱلْأَنْعَـٰمِ إِلَّا مَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ غَيْرَ مُحِلِّى ٱلصَّيْدِ وَأَنتُمْ حُرُمٌ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ يَحْكُمُ مَا يُرِيدُ ١

{1} Hii ni amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake Waumini juu ya yale ambayo yantakiwa na imani ya kutimiza mapatano. Yaani, kwa kuyakamilisha na kuyatimiza na kutoyavunja na kuyapunguza. Na hili linajumuisha mapatano ambayo yako baina ya mja na Mola wake Mlezi kama vile kushikamana na kumfanyia ibada, na kuzitekeleza kwa ukamilifu zaidi na kutopunguza kitu katika haki zake. Na zile ambazo ziko baina yake na Mtume kwa kumtii na kumfuata. Na zile ambazo ziko baina yake na wazazi wake na jamaa zake kwa kuwafanyia wema, na kuwaunga na kutowakata. Na zile ambazo ziko baina yake na wenza wake kama vile kutimiza haki za usuhuba katika utajiri na umasikini, na wepesi na dhiki. Na zile ambazo ziko baina yake na viumbe kama vile miamala kama vile kuuziana na kuajiri na mfano wake. Bali pia kutimiza haki za Waislamu ambazo Mwenyezi Mungu alizifunga baina yao kwa kauli yake. "Hakika, Waumini ni ndugu" [kwa kunusuriana] juu ya haki, na kushirikiana juu yake, na kuungana baina ya Waislamu, na kutokatana. Basi jambo hili linajumuisha misingi ya dini na matawi yake. Yote hayo yanaingia katika mapatano ambayo Mwenyezi Mungu aliamrisha yatimizwe. [Na Aya hii inatumika kama ushahidi ya kwamba kanuni ya asili katika mapatano na masharti ni kuruhusiwa, na kwamba yanahitimika kwa kile kinachoyaashiria kama vile maneno au kitendo kwa sababu hilo halikufungiwa kwa kizuizi ili chochote]. Kisha akasema kwa akiwakumbusha waja wake neema yake juu yao, "Mmehalalishiwa," yaani, kwa sababu ya kuwafanyia rehema, "wanyama wa kufugwa." Kama vile ngamia, na ng'ombe, na kondoo, bali pengine hata wakaingia ndani ya hilo wanyama pori, na swara, na punda pori, na mfano wao miongoni mwa wanyama wanaowindwa. Na baadhi ya Maswahaba waliitumia aya hii kama ushahidi wa kuruhusiwa kwa kijusi kinachokufia ndani ya tumbo la mama yake baada ya kuchinjwa kwa mamake. "Isipokuwa wale mnaosomewa," uharamu wake miongoni mwake katika kauli yake. "Mmeharimishiwa mizoga, na damu, na nyama ya nguruwe..." mpaka mwisho wa Aya. Kwani haya yaliyotajwa, hata ikiwa ni ya wanyama wa kufugwa, lakini ni marufuku. Na kwa kuwa kuruhusiwa kwa wanyama wa kufugwa ni kwa ujumla katika hali zote na nyakati zote, akatoa katika hilo uwindaji wakati wa ihram. Akasema, "Lakini msihalalishe kuwinda nanyi mmo katika Ihram." Yaani, mmehalalishiwa wanyama wa mifugo katika kila hali isipokuwa pale mnapokuwa mnasifika kuwa mnahalalisha kuwinda hali ya kuwa mko katika Ihram. Yaani, mnathubutu kumuua katika hali ya Ihram. Kwani hilo haliruhusiki kwenu ikiwa ni mawindo kama vile swara na wengineo. Na windo ni mnyama mwitu anayeliwa. "Hakika Mwenyezi Mungu anahukumu apendavyo," basi chochote anachotaka Mwenyezi Mungu; analohukumu kwalo hukumu inayoafikiana na hekima yake. Pia aliwaamrisha kutimiza mikataba; ili kufikia masilahi yenu, na kuwazuia na madhara. Na aliwahalalishia wanyama wa mifugo kwa sababu ya rehema yake juu yenu, na akawaharamishia yale aliyoyatoa katika uhalali huo miongoni mwa wale kasoro. Kama vile nyamafu na mfano wa hayo ili kuwahifadhi na kuwaheshimu, na vile vile uwindaji katika hali ya ihramu kwa sababu ya kuiheshimu na kuitukuza.