الزخرف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَٱصْفَحْ عَنْهُمْ وَقُلْ سَلَـٰمٌ ۚ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ ٨٩
{89} Ndiyo maana akasema: "Basi wasamehe, na uwaambie maneno ya salama." Yaani: Wasamehe kwa udhia wao wa kimaneno na wa kimatendo, wala usiwape chochote isipokuwa salama ambayo wenye akili na maono mazuri wanakutana kwayo wajinga. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu waja wake wema: "na wajinga wakiwasemeza hujibu: Salama!" Basi yeye - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alitekeleza amri ya Mola wake Mlezi, na akakutana na udhia uliomfikia kutoka kwa watu wake kwa msamaha na kuachilia mbali, na wala yeye amani iwe juu yake, hakukabiliana nao ila kwa kuwafanyia wema na kuwaongelesha maneno mazuri. Basi rehema na amani ziwe juu ya yule ambaye Mwenyezi Mungu aliyempa yeye tu tabia njema kuu ambayo kwayo alishinda wakazi wa ardhini na mbinguni, na akainuka kwayo juu kuliko nyota za kundinyota Mapacha (Juaza). Na kauli yake: "Watakuja jua" ubaya wa dhambi zao na mwisho wa uhalifu wao.
Imekamilika tafsiri ya surat Az-Zukhruf, na sifa njema zote na neema ni za Mwenyezi Mungu.