غافر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِٱلْكِتَـٰبِ وَبِمَآ أَرْسَلْنَا بِهِۦ رُسُلَنَا ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ ٧٠ إِذِ ٱلْأَغْلَـٰلُ فِىٓ أَعْنَـٰقِهِمْ وَٱلسَّلَـٰسِلُ يُسْحَبُونَ ٧١ فِى ٱلْحَمِيمِ ثُمَّ فِى ٱلنَّارِ يُسْجَرُونَ ٧٢
{70 - 72} Basi ni maovu kabisa waliyoyabadili na wakajichagulia wenyewe kwa kukikadhibisha Kitabu kilichowajia kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwatuma kwayo Mitume wake, ambao ndio bora wa viumbe wote, wakweli wao zaidi na wenye akili bora zaidi yao wote. Basi watu hawa hawana malipo yoyote ila Moto wenye mwako mkali. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akawatishia kwa adhabu yake, akasema: "Basi watakuja jua zitakapokuwa pingu shingoni mwao" wakashindwa kutembea nazo, "na minyororo" ambayo wao na mashetani wao wataunganishwa pamoja "huku wanabururwa Katika maji ya moto, kisha wanaunguzwa Motoni." Kisha watakaripiwa juu ya ushirikina wao na uwongo wao.