انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · غافر
السورة ٤٠

غافر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٧٣–٧٤

ثُمَّ قِيلَ لَهُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ تُشْرِكُونَ ٧٣ مِن دُونِ ٱللَّهِ ۖ قَالُوا۟ ضَلُّوا۟ عَنَّا بَل لَّمْ نَكُن نَّدْعُوا۟ مِن قَبْلُ شَيْـًٔا ۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ ٱللَّهُ ٱلْكَـٰفِرِينَ ٧٤

{73 - 74} Wataambiwa: "Wako wapi wale mliokuwa mkiwashirikisha. Badala ya Mwenyezi Mungu?" Je, waliwanufaisha au kuwaondolea baadhi ya adhabu? "Watasema: Wametupotea" na hawapo hapa, na hata wangehudhuria, hawangetusaidia kitu. Kisha wakakataa waliyofanya, wakasema: "Bali tangu zamani hatukuwa tukiomba kitu!" Inawezekana kwamba kilichokusudiwa na kukataa kwao huku ni kwamba walidhani kuwa huko kutawanufaisha kitu, na pia inawezekana kwamba - na hii ndiyo maana yake ya dhahiri zaidi - kwamba walikusudia kukiri ubatili wa uungu wa yale waliyokuwa wakiyaabudu, na kwamba hao si washirika wa Mwenyezi Mungu kwa uhakika, bali walipotea na wakakosea kwa kuabudu kisichokuwa na uungu wowote. Hii maana inaashiriwa na kauli yake Mola Mtukufu: "Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anawapoteza makafiri" kiasi kwamba wao wenyewe watakiri ubatilifu wake Siku ya Kiyama, na itawadhihirikia maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na wala hawawafuati hao wanaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu kuwa ni washirika wake; Wao hawafuati ila dhana tu." Na hayo yanaashiriwa na kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu: "Na Siku ya Kiyama watakataa ushirikina wenu." Na kauli yake: "Na ni nani mpotofu mkubwa kuliko hao wanaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu, ambao hawatawaitikia mpaka Siku ya Kiyama." Hadi mwisho wa Aya hizi.