انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · غافر
السورة ٤٠

غافر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٣٦–٣٧

وَقَالَ فِرْعَوْنُ يَـٰهَـٰمَـٰنُ ٱبْنِ لِى صَرْحًا لَّعَلِّىٓ أَبْلُغُ ٱلْأَسْبَـٰبَ ٣٦ أَسْبَـٰبَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ فَأَطَّلِعَ إِلَىٰٓ إِلَـٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّى لَأَظُنُّهُۥ كَـٰذِبًا ۚ وَكَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِفِرْعَوْنَ سُوٓءُ عَمَلِهِۦ وَصُدَّ عَنِ ٱلسَّبِيلِ ۚ وَمَا كَيْدُ فِرْعَوْنَ إِلَّا فِى تَبَابٍ ٣٧

{36 - 37} "Na Firauni akasema" akimpinga Musa na akikadhibisha wito wake wa kumkiri Mola Mlezi wa walimwengu wote, aliyeinuka juu ya Kiti cha Enzi na aliyetukuka juu ya viumbe vyote: "Ewe Hamana! Nijengee mnara" mkubwa mrefu ili nipate kuzifikia njia. "Njia za mbinguni ili nikamwone Mungu wa Musa. Na kwa hakika mimi bila ya shaka namjua kuwa ni mwongo tu" katika wito wake kwamba tuna Mola Mlezi, na kwamba yuko juu ya mbingu. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema katika kubainisha kilichompelekea kusema hivyo: "Na hivi ndivyo Firauni alivyopambiwa ubaya wa vitendo vyake" na Shetani akaendelea kumpambia hayo, kwa hivyo akawa anayalingania na kuyafanya kuonekana kuwa mazuri mpaka akayaona kwamba ni mazuri, akayalingania na akajadili mjadala wa mwenye haki, ilhali yeye ndiye mharibifu mkubwa zaidi. "Na akazuiliwa Njia" ya haki kwa sababu ya batili aliyopambiwa. "Na vitimbi vya Firauni" ambavyo alitaka kuipangia njama haki na kuwafanya watu kudhania kuwa yuko katika haki na kwamba Musa yuko katika batili "havikuwa ila katika kuangamia tu," wala havinufaishi isipokuwa kujitia mashakani katika dunia na akhera.